Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa amewaomba radhi watanzania kwa matokeo mabaya waliyoyapata katika mechi za kufuzu fainali za kombe la dunia baada ya kupokea kipigo kikubwa cha ba 7-0 dhidi ya Algeria.
Mkwasa amesema kwa niaba ya benchi zima la ufundi pamoja na wachezaji wanaomba radhi kwa matokeo hayo ambayo yamewaumiza watanzania ambao kwa asilimia kubwa wamekuwa wakiiunga mkono timu hiyo.
Mkwasa amesema licha ya kukosa uzoefu na ubora wa Algeria lakini walikutana na wakati mgumu kufuatia hujuma za wapinzani walizozifanya ndani na nje ya uwanja huku akigusia juu ya kumwagiwa maji kwa uwanja iliyopeleka wachezaji wake kuteleza pia maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo aliyekua akionekana kuwasikiliza zaidi wachezaji wa Algeria.
Nae nahodha msaidizi wa kikosi hicho John Bocco Adebayro amesema nia yao ilikua kuibuka na ushindi ila matokeo yakawa kinyume na walivyotarajia hivyo watajipanga katika mashindano mengine yaliyo mbele yetu.
Kwa pamoja Mkwasa na Bocco wamesema matokeo hayo yamekuwa ni funzo kwao na watanzania kwa ujumla kuhakikisha wanaangalia namna ya kujikwamua hapa tulipoo kwa kuangalia misingi ya kuboresha soka la hapa nchini kama ilivyo kwa mataifa yaliyoendelea.
Social Plugin