LIPUMBA AIBUKIA OFISI ZA CUF!! AFUNGUKA MAZITO KINACHOENDELEA ZANZIBAR



Ibrahim Lipumba
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amemwomba Rais Jakaya Kikwete kuiamuru Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC ) kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa uliofanyika Zanzibar ili kuiepusha nchi kuingia katika machafuko.


Jumatano iliyopita, Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha alifuta matokeo ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu akisema uchaguzi ulikuwa na kasoro nyingi.

Akizungumza jana kwa mara ya kwanza na waandishi wa habari tangu alipojiuzulu, Agosti 6, mwaka huu, Lipumba alisema amelazimika kutoa ushauri baada ya kuona hatari iliyo mbele kama wananchi wa Zanzibar watanyang’anywa haki yao.

“Ijumaa ijayo Dk John Magufuli ataapishwa kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Tanzania, Kikwete usimwongezee Magufuli matatizo yaliyopo yanamtosha, ” alisema.

Lipumba ambaye alipokelewa na wafuasi zaidi ya 100 kwenye ofisi za chama hicho zilizopo Buguruni, alisema Kikwete ahakikishe kabla hajamaliza muda wake wanaiamuru ZEC kuendelea kutangaza matokeo na kuwatangaza washindi wa uchaguzi huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post