Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NDUGAI CCM AIBUKA MSHINDI USPIKA WA BUNGE APATA KURA 254, MEDEYE WA CHADEMA 109, WENGINE 0







Wabunge wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania leo Mjini Dodoma wamemchagua mheshimiwa Job Yustino Ndugai kuwa spika wa bunge la Jamhuri wa muungano wa Tanzania.

Katibu wa Bunge Mh Dkt Thomasi Kashilila Amemtangaza Mh Job ndugai kuwa Spika wa Bunge la 11 baada ya Kujinyakulia Kura 254 sawa na 70% ya Kura zote zilizopigwa.


Mh Ndugai amewashinda Wagombea wengine kutoka vyama na makundi Mbalimbali

Matokeo ya kura za Spika.

A: Job Ndugai (CCM)- 254
B: Goodluck Ole Medeye (CHADEMA) - 109
C: Hashimu Rungwe (CHAUMA)- 0
D: Peter Sarungi (AFP) -0
E: Dkt Godfrey Malisa (CCK)- 0
F: Richard Lymo (T.L.P) -0
G: Robert Kisinini (DP) -0

Kura zilizoharibika ni 2



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com