Wananchi wakishangaa kiumbe hicho |
Wananchi wakiwa eneo la tukio
Mkazi wa kata ya Goweko, Wilaya ya Uyui,mkoani Tabora Hadija Ramadhan amejifungua kiumbe cha ajabu kinachofanana na mbweha.
Kiumbe hicho kilikuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa kijiji hicho na maeneo ya jirani ambao walisafiri hadi kijijini hapo kwenda kushuhudia.
Diwani mteule wa kata ya Goweko Shaban Katalambula alisema kiumbe kilichozaliwa kinafanana na Mbweha ambacho kilizaliwa na baada ya muda kidogo kilifariki.
Kwa upande wa mkunga aliyemzalisha mwanamke huyo Hobokela Mwasisya alisema kiumbe hicho cha ajabu kilizaliwa juzi saa 3 na kufariki muda mchache baadaye.
Alisema mwanamke huyo ambaye ni uzao wake wa tano alienda katika zahanati hiyo akilalamika kuumwa tumbo lakini wakati wa kujifungua hakutokwa damu jambo lililowashangaza wananchi hadi alipokimbizwa hospitali ya Mkoa kwa uchunguzi zaidi.
Social Plugin