Jana katibu mkuu wa Wizara ya afya Dk.Donan Mmbando alizungumzia kuhusu mikakati ya kutaka kufunga maduka ya dawa yaliyo karibu na hospitali za Serikali kwa madai ya malalamiko ya wizi wa dawa hizo kutoka hospitali.
Leo Msemaji wa Wizara hiyo Nsachris Mwamwaja amezungumzia moja ya mikakati ya Wizara hiyo ni pamoja na kuhakikisha kunakuwepo na maduka ya dawa ndani ya hospitali ambayo yatakuwa ya Serikali chini ya Bohari kuu ya dawa MSD.
“Hospitali ya Muhimbili ina maduka ya dawa ndani, tumepanga kuhakikisha kila hospitali ya Serikali inakuwa na duka ndani, na tutahakikisha dawa zote zitakuwepo, lengo ni kuondoa malalamiko ya watu kuwa yale maduka ndio chanzo cha kukosekana kwa dawa mahospitalini”...Nsachris Mwamwaja
“Ni kweli haya maduka yapo sehemu ambazo wauguzi ndio hutoa maelezo wagonjwa wakanunue hizo dawa katika maduka hayo, wagonjwa wanaotumia huduma za mifuko ya jamii pia watakuwa wakitumia maduka ya hospitali za Seeikali, nia yetu ni wagonjwa wapate dawa bila usumbufu wowote”..
Kingine kilichosikika kutoka ndani ya Wizara hiyo ni utapeli ambao umekuwa ukifanywa kwa waajiri ambapo kumejitokeza wimbi la matapeli na kuwapangia watu maeneo ya kwenda kufanya kazi kitu ambacho si kweli kwa kuwa Wizara hiyo haijatoa majina ya ajira na haijawapangia watu vituo vya afya.
“Kuna taratibu za kukufanya uingizwe kwenye mfumo wa kulipwa na Wizara, ni ngumu kuingia kirahisi huo ni udanyangifu unaofanywa na baadhi ya watu ambao si waaminifu katika baadhi ya ofisi..pia wizara haitoa barua wala kuajiri bali inatoa majina na kupeleka kwa waajiri husika”…