MAGUFULI AAGIZA PESA ZA SHEREHE YA WABUNGE ZIKASAIDIE MUHIMBILI,ZIKO HAPA SENTENSI ZAKE ZA HATARI
Saturday, November 21, 2015
Rais John Pombe Magufuli ameagiza kuwa fedha zilizochangwa kwa ajili ya sherehe iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili ya wabunge na yeye kualikwa, zipelekwe katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Magufuli ametoa agizo hilo baada ya kuhudhuria sherehe hiyo na kupokea taarifa kuwa kiasi cha shilingi milioni 225 kilikuwa kimechangwa na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za kibenki kwa ajili ya sherehe hiyo ya uzinduzi wa bunge
Kwa mujibu wa Afisa wa Bunge Bw. Said Yakubu, Rais Magufuli ameagiza katika sherehe hiyo zitumike shilingi milioni 24 pekee na nyingine ziende Muhimbili zikasaidie kununua vitanda ili kupunguza tatizo la wagonjwa kulala chini.
Yakubu amesema kuwa agizo hilo la Rais limetekelezwa.
Ziko hapa Sentensi kadhaa za Rais John Pombe Magufuli akiwa Bungeni Dodoma
Rais @MagufuliJP : Yote tuliyowaahidi tutayafanya kwelikweli, sikuahidi ili nipigiwe kura bali ili kuyatimiza yote
Rais @MagufuliJP : Siku ya Tarehe 25 Oktoba ilikuwa ni ya furaha sana, kuna watu walifikiri tutafarakana lakini wameshangaa
Rais @MagufuliJP : Nampongeza @zittokabwe kwa kuonesha utulivu, yeye hakupiga kelele, nahitaji Tanzania ya aina hii
Rais @MagufuliJP :Kati ya maeneo mengi yaliyolalamikiwa kwenye kampeni ni RUSHWA,lingine ni upotevu wa fedha za halmashauri
Rais @MagufuliJP : Eneo lingine ni tatizo la maji, na lingine ni TRA kushindwa kukusanya kodi na kuachia ukwepaji kodi
Rais @MagufuliJP : Eneo lingine ni migogoro ya ardhi, TANESCO, huduma za afya na Maliasili
Rais @MagufuliJP : Haiwezekani meno ya tembo yakamatwe nchi za watu huko bila watu wa idara husika kuhusika
Rais @MagufuliJP : Suala lingine ni kuhusu elimu, viwanda n.k Ni lazima niyaseme haya ili tujue wapi tunaanzia
Rais @MagufuliJP : Mimi ni muumini wa muungano, niliapa kuulinda muungano, hata nisipoapa, ni lazima niulinde muungano
Rais @MagufuliJP : Suala lingine ni kuimarisha miimili ya serikali, serikali itahakikisha miimili yote inaimrika.
Rais @MagufuliJP : Kwa upande wa bunge tutahakikisha fedha za mfuko wa bunge zinapatikana kwa wakati
Rais @MagufuliJP : Kuhusu Katiba, nimepokea kiporo kutoka kwa serikali ya awamu ya 4, tutarekebisha sheria katiba ipatikane
Rais @MagufuliJP : Kuhusu uchumi, tutaimarisha miundombinu iliyopo na kujenga mipya ili kuvutia wawekezaji
Rais @MagufuliJP : Kuhusu viwanda, serikali ya awamu ya tano itaweka uzito mkubwa katika viwanda. Natambua wawekezaji
Rais @MagufuliJP :Tutaanza na viwanda vilivyopo na kuhakikisha vinafanya kazi, waliokuwa hawaviendelezi niliwataka kuviacha
Rais @MagufuliJP :Hatuwezi kuwa na watu wanajiita wawekezaji, tunawapa viwanda vyetu halafu wanaviatamia tu kama mayai
Rais @MagufuliJP : Kuna wengine wameamua hata kufugia mbuzi majengo ya viwanda vyetu
Rais @MagufuliJP : Watendaji wa serikali watakaosababisha vikwazo kwa wawekezaji hatutakuwa na nafasi zao
Rais @MagufuliJP : Sura ya tatu ya viwanda ni kuzalisha ajira nyingi, nataka sekta ya viwanda ichangie 40% ya ajira zote
Rais @MagufuliJP : Tutazingalia sekta za mifugo, kilimo na uvuvi kwa jicho la kibishara, watanzania wengi wanazitegemea
Rais @MagufuliJP : Makodi yote ya ovyo ovyo ambayo ni kero kwa wakulima wetu tutayaondoa kama si kuyapunguza yote
Rais @MagufuliJP : 28.2% ni masikini, lazima tushughulikie umasikini kwa kupunguza tofauti kati ya walionacho na wasionacho
Rais @MagufuliJP : Hatuwezi kuendeleza viwanda ikiwa hatujawekeza kwa vijana kwa kuwapa ujuzi na maarifa
Rais @MagufuliJP : Tutahakikisha shule na vyuo vyetu vinaandaa vijana wenye uwezo, ujuzi na maarifa na watapatiwa mikopo.
Rais @MagufuliJP : Tutawawezesha vijana kujitafutia maisha yao kama vile bodaboda, mama lishe, machinga n.k
Rais @MagufuliJP : Kodi ambayo haikusanywi ni nyingi na ingeweza kuendesha nchi, lakini tunahangaika na watanzania wanyonge
Rais @MagufuliJP :Kila kijiji kitakuwa na zahanati, kila kata kitakuwa na kituo cha afya na kila wilaya hospitali ya wilaya
Rais @MagufuliJP :Tutaboresha huduma za afya maana imekuwa ni mazoea mtu akiugua hata mafua anaenda kutibiwa nje ya nchi
Rais @MagufuliJP : Kuanzia Januari mwakani wanafunzi watasoma bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.
Rais @MagufuliJP : Dawa za kulevya. Tutakabiliana na mtandao mkubwa wa madawa ya kulevya, tutatafuta wale wahusika wakubwa
Rais @MagufuliJP : Nachukizwa sana na vitendo vya rushwa na ufisadi, vitendo hivi vinawatia hasara kubwa sana watanzania
Rais @MagufuliJP : Chama changu cha @ccm_tanzania kimejengwa katika misingi ya kuchukia rushwa na ufisadi,
Rais @MagufuliJP : Sina uhakika kama sasa ndani ya CCM hakuna watu wanaotoa na kupokea rushwa
Rais @MagufuliJP : Dawa ya jipu ni kulitumbua, na mimi nimejipa kazi ya kuwa MTUMBUA MAJIPU, naomba wabunge mniunge mkono
Rais @MagufuliJP : Ili kusimamia kazi ya kutumbua majipu nimesema nitaanzisha mahakama ya rusha na mafisadi
Rais @MagufuliJP : Kama nimeteua mtu yoyote halafu nikabaini kuwa anahusika na vitendo vya rushwa na ufisadi NITAMTIMUA
Rais @MagufuliJP : Watendaji wazembe hawatavumiliwa katika serikali yangu, tumewavumia vya kutosha, wakati sasa umekwisha
Rais @MagufuliJP : Tutahakikiksha kila mtu anayestahili kulipa kodi, analipa kodi, unaponunua bidhaa yoyote dai risiti
Rais @MagufuliJP : Tutahakikisha safari zote za nje ya nchi zinadhibitiwa ili kuongeza mapato
Rais @MagufuliJP : Katika mwaka 2013/14 zaidi ya bilion 300 zilitumika kwa safari za nje na zingeweza kuwatumikia wananchi
Rais @MagufuliJP : Idara zilizoongoza kwa safari za nje ni Bunge, mambo ya nje, Wizara ya Fedha, Wizara ya mambo ya ndani
Rais @MagufuliJP :Pia tunazuia ziara za mafunzo nje ya nchi, huyo mnayeenda awafundishe kwanini msimuite aje hapa kwetu
Rais @MagufuliJP : Kuna watu hapa wameshasafiri nje ya nchi mara nyingi zaidi kuliko walivyosafiri kwenda kwa wazazi wao
Rais @MagufuliJP : Sheria ya manunuzini mbaya, unaweza kukuta kalamu ya Bic inayouzwa Tsh. 1000 inanunuliwa kwa Tsh. 10,000
Rais @MagufuliJP : Bunge ni chombo muhimu, halipaswi kuwa chombo la mipasho, kutukanana, kutoka nje, n.k
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin