Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAN CITY, REAL MADRID ZAPIGWA 4 KILA MOJA





Real Madrid imekumbana na kipigo cha aina yake kutoka mahasimu wao katika soka la Hispania klabu ya Barcelona katika mchezo wa ligi kuu Hispania uliopigwa leo katika dimba la Santiago Bernabeu.

Katika mchezo huo maarufu kama El Clasico, Barcelona imepata ushindi wa mabao 4-0 yakifungwa na Suarez dakika za 11 na 74, Neymar dakika ya 39 na Iniesta dakika ya 53.

Vikosi vya timu zote vilikuwa vimekamilika huku Lionel Messi akiingia kipindi cha pili.

Nchini Uingereza Liverpool imeishushia kipigo cha mabao 4-1 Man City katika dimbala Itihad,

Mabao ya Liverpool yamefungwa na Mangala dakika 8 likiwa ni la kujifunga, Coutinho 23, Firmino 32 na Skrtel dakika ya 81.

Bao la Man City limefungwa na Aguero dakika ya 44.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com