Mchekeshaji, Masanja Mkandanizaji ameangukia pua katika kura za maoni za ubunge katika jimbo la Ludema baada ya kupata kura chache.
Deo Ngalawa aliwashinda makada wenzake tisa waliokuwa wakiwania nafasi hiyo kwa kupata kura 537 akifuatiwa na mdogo wa marehemu Filikunjombe, Philip aliyepata kura 501.
Makada wengine ni Edgar Lugome, Johnson Mgimba, Emmanuel Mgaya maarufu Masanja Mkandamizaji (19), James Mgaya (72), Jackob Mpangala (3), Evaristo Mtitu (21) na Zephania Chaula (38).
.
Sasa Deo Ngalawa kuvaa kiatu cha aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe(CCM) aliyefariki kwa ajali ya helkopita siku chache kabla ya uchaguzi Tanzania 2015