Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MATOKEO YA MCHEZO WA LEO SOMALIA vs KILIMANJARO STARS CECAFA 2015



November 22 michuano ya mataifa ya Afrika Mashariki na kati maarufu kama CECAFA iliendelea kwa michezo miwili kupigwa, timu ya taifa ya Tanzania bara ambapo inafahamika kama Kilimanjaro Stars ilishuka dimbani kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Somalia.

Kilimanjaro Stars ambayo ndio imecheza mchezo wake wa kwanza leo November 22 ikiwa na tahadhari au kumbukumbu ya kilichowakuta ndugu zao Zanzibar Heroes ambao walipoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya timu ya taifa ya Burundi kwa goli 1-0.



Stars ambao wapo chini ya kocha King Kibadeni walifanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya goli 4-0 dhidi ya Somalia ambao wamekuwa hawana rekodi nzuri katika soka, magoli ya Kilimanjaro Stars yalifungwa na nahodha wao John Bocco kwa mkwaju wa penati dakika ya 12, Elias Maguli dakika ya 17 na 54 na dakika moja baadae John Bocco akapachika tena goli la nne.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com