Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MCHUNGAJI WA KANISA AWALISHA NYOKA NA NGUO ZA NDANI "CHUP" WAUMINI WAKE....KANISA LAKE LACHOMWA MOTO,VIDEO IKO HAPA



Hizi stori kutoka kwa viongozi wa nyumba za ibada kuwa na matendo yanayoibua maswali mengi sio ngeni masikioni mwetu, nimeinasa nyingine toka South Africa, Mchungaji kawalisha Waumini wake nyoka pamoja na nguo za ndani..



Mchungaji huyo Penuel Mnguni ambaye ni Kiongozi wa Kanisa la End Times Disciples Ministries lililopo katika Mji wa Soshanguve ulioko Pretoria South Africa, alijikuta akiishia mikononi mwa watu wenye hasira na matendo yake, huku Kanisa lake likiteketea baada ya kuchomwa moto na watu haohao !!



Taarifa zilienea mitaani kuhusu huduma zake, alikuwa akiwalazimisha waumini wake kula nyoka pamoja na nguo za ndani kama sehemu ya huduma za Kanisa lake kwa Waumini… watu wa eneo hilo waliwavamia na kumkamata Mchungaji huyo, Kanisa likaishia kuchomwa moto, ambapo baada ya muda kidogo ilibidi Polisi waingilie kati kumuokoa.

Video ya tukio lenyewe hii hapa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com