Mtafaruku!!! JENGO LA KITALII LAANGUKA ZANZIBAR...CHANZO MVUA NA UPEPO





Paa la jengo la Beit-al-ajab moja ya kivutio kikubwa cha utalii Zanzibar limeanguka na kusababisha mtafaruku mkubwa kwa wakazi wa Mjimkongwe. 
 
 
Paa hilo limeanguka baada ya kuwepo mvua na upepo mkali ambao ulianza wakati wa asubui na paa hilo lililoko kwenye jengo hilo la ghorofa tatu kuanguka chini na kuharibu gari tatu zilizokuwa zimeegeshwa na mshutuko huo kusababisha watu kukimbia na kuacha mali zao za biashara hata hivyo hakuna athari za kuumia binadamu.

Baadhi ya mashuuda walioshuudia paa hilo likianguka wamesema ajali hiyo ilitokozea ghafla na kilichosaidia na kwanza kuwepo kwa sauti ya mshtuko na baadaye ndiYo paa hilo likaanza kuanguka hali hiyo ndiyo iliyosaidia watu waliokuwa wameketi chini na wafanyabiashara za watalii.

Naye mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hifadhi wa Mjimkongwe Zanzibar Bw Issa Sarboko akiongea kwenye eneo la tukio amesisitiza kuwa jengo hilo ni madhubuti na halijaathirika kilichotokea ni kuwepo mwanya wa upepo lakini mamlaka inalishugulikia ili kuondosha tatizo lakini kwa hivi sasa jengo ilo limefungwa kwa ajli ya ukarabati.

Jengo hilo la Beita ajab ambalo ni moja ya kivutio kikubwa cha watalii Zanzibar, hii ni mara ya pili ya kuwepo kwa ajali za kuporomoka kwa jengo hilo ambalo limekuwepo zaidi ya miaka 100 na lilikuwa ni jengo la ofisi kuu za serikali kabla ya mapinduzi na hivi sasa ni makumbusho kubwa la historia ya Zanzibar.
 
Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post