Mgombea wa nafasi ya Spika wa Bunge la 11, Job Ndugai, amejitabiria magumu katika Bunge hilo kwa kueleza kuwa litakuwa ni lenye changamoto nyingi ambazo atahakikisha anazimudu.
Kadhalika, ameweka bayana magumu ya Bunge hilo kuwa ni uwapo wa wabunge wengi wa upinzani, wabunge wasomi kuliko mabunge yaliyopita na kwamba kuna uwezekano wa kuwa na migomo ya hapa na pale.
Akizungumza na waandishi wa habari, baada ya kutangazwa kupewa idhini na Chama Cha Mapinduzi kupeperusha bendera yake katika uchaguzi wa Spika, alisema anatambua kuwa Bunge hilo litakuwa ni lenye mabadiliko makubwa tofauti na mabunge yaliyopita.
“Kuna ongezeko la vijana, wapinzani na wabunge wengi ni wasomi tofauti na mabunge yaliyopita, hivyo uendeshaji wake ni lazima ubadilike. Natambua changamoto nyingi zilizopo mbele tutarajie migomo mingi, lakini tutegemee Bunge lenye kuishauri na kusimamia serikali,” alisema.
Ndugai ambaye pia ni Mbunge Mteule wa Kogwa, alisema Bunge lijalo atalisimamia lifanye kazi kwa viwango vinavyotakiwa kwa kuwa hakikisha wanawatumikia Watanznaia.
“Nitatenda haki kwa Wabunge wote, nitasimamia haki kwa vyama vyote, hakuna ambaye hatapata haki mbele ya kiti cha Spika, nawaomba wote waniunge mkono na wanipe kura nyingi za ushindi ili imani yangu kwao izidi,” alisema.
Alieleza kuwa alipokuwa Naibu Spika alifanya kazi kwa haki na kwa sasa atahakikisha kila mbunge anapewa kipaumbele cha fursa ya kuhakikisha anatoa hoja yake.
Ndugai alisema kaulimbiu yake atakayoisimamia ni ‘Sasa Kazi tu’ inayotimiwa na Rais John Magufuli, na kwamba Bunge lijalo litakidhi matarajio ya Watanzania.
NAPE
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akizungumza na waandishi wa habari, alisema wabunge wateule kwa kauli moja walipitisha jina la Ndugai, baada ya wagombea wenzake kujitoa.
“Tulivyoanza kikao tu wagombea Dk. Tulia Ackson na Abdallah Ali Mwinyi, walitangaza kujitoa na kumuachia Ndugai, wabunge wateuele kwa kauli moja walimpitisha na kuonyesha kuwa ameshinda kwa asilimia 74.8,” alisema na kuongeza:
“Tunaamini huyu ndiye Spika kwa kuwa Bunge la 11 wabunge wa CCM ni asilimia 74.8, hivyo moja kwa moja huyu ndiye mshindi…sifa za Ndugai zinatosha kumpa ushindi, hakuna mgombea aliyeonyesha kazi zake kwa vitendo kama huyu.”
Alisema wagombea wenzake walijitoa baada ya kueleza kuwa wanaamini uwezo wa Ndugai hawalingani nao, hivyo wakamuachia nafasi hiyo.
Nape alisema jina hilo litapelekwa kwa uongozi wa Bunge kwa ajili ya kumshindanisha leo na wagombeawa vyama vingine.
WAGOMBEA WENGINE
Ofisi ya Bunge imesema imepokea majina nane ya wagombea wa nafasi ya Spika kutoka vyama kadhaa vya siasa.
Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah, alisema wagombea hao ndiyo walioteuliwa kugombea nafasi hiyo leo, baada ya kumalizika kwa muda wa kupokea majina jana saa 10 jioni.
Aliwataja wagombea hao na vyama vyao kwenye mabano kuwa ni Peter Sarungi (AFP), Hassan Kisabya (NRA), Dk. Godfrey Malisa (CCK), Job Ndugai (CCM), Dk. Goodluck Medeye (Chadema), Macmillian Lyimo (TLP), na Hashim Rugwe (Chaumma) na Robert Kasini (DP).
Dk. Kashilillahalisema maandalizi yote muhimu ya Mkutano wa Kwanza wa Bunge la 11 Bunge yamekamilika.
“Hadi saa 10 jioni tumesajili wabunge 348, taratibu zote ndani ya ukumbi zimekamilika tutaanza na uchaguzi wa Spika ambaye atakula kiapo na kuendelea kuwaapisha wabunge,” alisema.
Jumla ya wabunge wa majimbo ni 257 yaliyofanya uchaguzi mkuu. Majimbo saba hayajafanya uchaguzi, wabunge waliosajiliwa ni 348 kati ya wabunge 367 wanaotakiwa kuwapo katika Bunge hilo.
WABUNGE/WAGOMBE WAMZUNGUMZIA
Baadhi ya wabunge wateule na viongozi wa CCM, wamemzungumzia Ndugai kuwa ndiye mtu sahihi kwa Bunge la 11, ambalo lina changamoto nyingi zinazohitaji mtu mzoefu wa nafasi hiyo.
Mbunge wa Ngara, Gashaza Alex, alisema ana uhakika Ndugai ana uzoefu wa kutosha katika nafasi aliyoomba, kinachotakiwa ni kumuuga mkono.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Adamu Kimbisa, alisema Ndugai ni mwenye kujali makundi yote na ndiyo maana katika vikao vya Bunge la 10 wapinzania aliwatendea haki bila kujali itikadi zao.
“CCM imepata mtu sahihi na ndiyo maana amepitishwa bila kupingwa, tuna matarajio makubwa sana kwake, na suala la migomo kwenye mabunge ni la kawaida ulimwenguni, tunaamini atatatenda haki kwa wote na kuwa na Bunge lenye kukidhi matarajio ya wengi,” alisema.
Mbunge Mteule wa jimbo la Peramiho, Jenister Muhagama, alisema Ndugai anatosha, ni mzoefu na wanaamini atakuwa Spika wa namna yake, kwa kuwa hataangalia wingi wa wabunge wa chama chake bali hoja za msingi.
Mbunge wa Viti Maalum, Zainabu Vullu, alisema ana uzoefu anaweza kuhimili mikikimiki iliyopo sasa, na ataendesha Bunge kwa kikudhi mahitaji ya chama na wananchi kwa kuzingatia kaulimbiu ‘Hapa Kazi Tu’, kwa Bunge lenye sura mpya.
Mbunge wa Kasulu Kusini, Husna Mwilima, alisema Ndugai anastahili kukabidhiwa jukumu hilo, kwa kuwa ataweza kutokana na uzoefu wa kazi hiyo kwa muda mrefu na kwamba wagombea waliogombea naye ndani ya CCM walitambua uwezo wake, ndiyo maana walitumia busara kujiondoa.
Dk. ACKSON
Akizungumza na waandishi wa habari, Dk. Tulia Ackson, alisema alijiondoa katika hatua ya mwisho, ingawa hakutaka kufafanua sababu za kujiondoa kwake.
“Ni kweli nimejiondoa, nitaongea baadaye kwa sasa niacheni,” alisema kwa kifupi na kuondoka.
RAIS MAGUFULI AMTEUA UBUNGE
Katika hatua nyingine, Rais John Magufuli, jana alimteua Dk. Ackson kuwa Mbunge wa Kuteuliwa.
Kutokana na hatua hiyo, Rais Magufuli alitengua uteuzi wake wa unaibu mwanasheria mkuu wa serikali, nafasi aliyoteuliwa siku za mwisho kabla ya Rais mstaafu, Jakaya Kikwete kuondoka madarakani.
NAIBU SPIKA
Ofisi Bunge imesema imepokea majina nane ya wagombea wa nafasi ya Spika wa Bunge la 11 la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari jana katika ofisi za Bunge, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilillah, alisema wagombea hao ndiyo walioteuliwa kugombea nafasi hiyo leo, baada ya kumalizika kwa muda wa kupokea majina jana saa 10 jioni.
Aliwataja wagombea hao na vyama vyao kwenye mabano ni Peter Sarungi (AFP), Hassan Kisabya (NRA), Dk. Godfrey Malisa (CCK), Job Ndugai (CCM), Dk. Goodluck Medeye (Chadema), Richard Lyimo (TLP), aliyekuwa mgombea urais wa Chaumma, Hashim Rugwe na Robert Kasini (DP).
Akizungumzia maandalizi ya kikao cha kwanza cha Bunge la 11, Dk. Kashilillah ambaye alikuwa ameambatana na Naibu Katibu wa Shughuli za Bunge, John Joel na Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge ( MSB), Nenelwa Mwihambi, alisema maandalizi yote muhimu yamekamilika.
"Hadi saa 10 jioni tumesajili wabunge 348, taratibu zote ndani ya ukumbi zimekamilika tutaanza na uchaguzi wa Spika ambaye atakula kiapo na kuendelea kuwaapisha wabunge," alisema.
Jumla ya wabunge wa majimbo ni 257 yaliyofanya uchaguzi mkuu, majimbo saba bado hayajafanya uchaguzi, wabunge waliosajiliwa ni 348 kati ya wabunge 367 wanaotakiwa kuwapo katika Bunge hilo.
UNAIBU SPIKA
Wakati huo huo, taarifa kutoka ndani ya kikao cha Wabunge wa CCM zinasema hadi jana jioni watu saba walijitokeza kuwania nafasi ya naibu Spika wakiwamo Dk. Tulia Ackson na Zungu.
Hata hivyo, katibu wa wabunge hao, Jenister Mhagama, hawakuwa tayari kuyataja kwa maelezo kuwa bado utaratibu unaendelea.
Mhagama alisema leo zitapigwa kura kupata jina moja la mgombea litakalowasilishwa bungeni
Imeandikwa na Salome Kitomari, Moshi Lusonzo na Agusta Njoji
CHANZO: NIPASHE

Social Plugin