Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

News Alert!! HAYA NDIYO MAAMUZI YA MAHAKAMA KUHUSU KUAGA MWILI WA KIGOGO WA CHADEMA ALIYEUAWA





Kumekuwepo na sintofahamu juu ya hatma ya kuuzika mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Geita Alponce Mawazo baada ya kutokea kwa mvutano kati ya UKAWA na Jeshi la Polisi.

UKAWA pamoja na ndugu wa marehemu jana waliamua kufungua kesi katika mahakama kuu ya Mwanza wakipinga kauli ya RPC wa Mwanza Charles Mkumbo aliyoagiza kusiwepo shughuli za kuaga mwili wa marehemu huyo kutokana na kuwepo Ugonjwa wa Kipindupindu kilichoibuka maeneo mbalimbali ikiwemo ndani ya Mwanza yenyewe.

Viongozi mbalimbali wa CHADEMA akiwemo Mbunge na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe na Mwanasheria wa Chama hicho, John Mallya walifika Mahakama Kuu Mwanza na kesi tayari imesomwa.

Leo mahakama kuu Mwanza imetoa maamuzi ya kusikilizwa kwa maombi ya familia ya marehemu Mawazo kuhusu ndugu yao kuweza kuagwa na kufuatwa kwa taratibu zote za mazishi, kwa sasa kesi hiyo inaendelea kusikilizwa.


Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Lameck Mlacha, ametupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na RPC wa Mwanza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya kesi iliyofunguliwa jana na familia ya Marehemu Alphonce mawazo kuomba tafsri ya mahakama baada ya jeshi la polisi mkoani Mwanza kupiga marufuku mikusanyiko ya kuuaga mwili wa marehemu.
 
Chanzo-Millardayo.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com