Katika pitapita zake kamera za Malunde1 blog zimewanasa watoto hawa wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 7 hadi 13 wakicheza mchezo wa kuruka sarakasi katika mtaa wa Mnara wa Voda mjini Shinyanga ikiwa ni utaratibu waliojiwekea wa kufanya mazoezi kila siku asubuhi,mchana na jioni kama walivyueleza Mtandao huu.Watoto hao wamesema wapo 10 na wameunda kundi lao walilolipa jina la "Child Dance" na wamekuwa wakifanya mazoezi hayo tangu mweza Januari mwaka huu..Picha na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Mtoto akiruka juu baada ya kukanyaga jiwe
Watoto hao walisema wanahitaji mfadhili atayewasaidia kuendeleza kipaji chao hivyo kama unapenda watoto na upenda kuendeleza watoto wasiliana na mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,bwana Kadama Malunde kwa simu namba 0757478553.Hawana uwanja wa kufanyia mazoezi bali hufanyia popote penye uwazi katika mtaa wa Mnara wa Voda..
Mtoto akiruka sarakasi juu ya mgongo wa mwenzake
Watoto wakionesha vipaji vyao...Picha na Kadama Malunde- Malunde1 blog