Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

POLISI MKOANI KATAVI WAKAMATWA WATUHUMIWA WAWILI WA UJANGILI WAKIWA NA MENO YA TEMBO YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 60




Jeshi la Polisi mkoani Katavi linawashikilia watuhumiwa wawili wa ujangili, waliokamatwa kwenye kijiji cha Usevya wilayani Mlele wakiwa na nyara za serikali kinyume cha sheria, vikiwa ni vipande vinne vya meno ya Tembo vyenye uzito wa zaidi ya kilo 45 na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 60, na vikiwa vimehifadhiwa kwenye mfuko wa sandarusi. 




Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Katavi kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Dhahiri Kidavashari, akithibitisha kuhusu tukio hilo mjini Mpanda amesema ushirikiano wao na askari wanyamapori wa hifadhi ya taifa ya Katavi, wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao wa ujangili aliowataja kuwa Justin Bruno na Philbert Leo wote wakazi wa kitongoji cha Tompolo tarafa ya Mpimbwe wilayani Mlele, wakiwa wamevihifadhi vipande hivyo kwenye mfuko wa sandarusi, na kuvipakia kwenye pikipiki aina ya toyo yenye namba za usajili T 645 CUS.

Kwa upande wao baadhi ya maafisa wa hifadhi ya taifa ya Katavi, akiwemo na kaimu mhifadhi mkuu wa hifadhi hiyo Bw Yustin Njamasi, wametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati katika operesheni inayoendelea hivi sasa ya kuwasaka majangili wanaoangamiza raslimali hiyo muhimu, inayoliingizia taifa fedha nyingi kwa njia ya utalii.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com