Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PROFESA LIPUMBA AIBUKA TENA- AMPA KAZI NZITO RAIS MAGUFULI KUHUSU ZANZIBAR NA DR SHEIN BUNGENI...KESHO UKAWA KUWASHA MOTO BUNGENI

ALIYEKUWA mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF,Profesa Ibrahimu Lipumba ameibuka tena,na sahivi amemtaka Rais John Magufuli kuiamuru Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kumtangaza Mgombea wa Urais kupitia CUF,Maalim Sef sharif Hamadi kuwa mshindi wa Nafasi ya Urais.

Profesa Lipumba ambaye alijiuzulu nafasi ya hiyo alikuwa nayo , miezi mine iliyopita kutokana na kutoelewana na Viongozi wa vyama vya UKAWA na Mkutano wake na wanahabari ulifanyika kwenye Hoteli moja hapa jijini ambayo inadaiwa gharama za hoteli hizo zililipwa na Chama Cha Mapinduzi CCM.
 
Leo Lipumba  ameibuka kwenye makao makuu ya Ofisi za chama hicho zilizopo Bururuni jijini hapa na kuzungumza na waandishi wa habari na kuzungumzia mgogoro mkubwa unaoendelea visiwani Zanzibar na kusema hali hiyo ikiendelea hivyo itaweza hata kuvuruga umoja ambao Taifa unao na kusababisha kukwamisha shuhguli zote za kimaendeleo.

“Namuomba Rais Magufuli aliokoe Taifa lilipofikia kwa kuiamuru ZEC kutangaza matokeo ya Urais yaliyobakia la sivyo,kama naye akiendelea kuacha uvunjifu wa Katiba ya Zanzibar basi Taifa halitaweza kusonga mbele litakuwa kila siku lipo kwenye mgogoro”,ameeleza Lipumba.
 
Amesema kitendo cha Rais Magufuli kwenda kulihutubia Bunge kesho na kuongozana na Rais wa Zanzibar anayedai amemaliza muda wake Dk Mohamed Shein hakikubaliki na kinakwenda kinyume na katiba ya Zanzibar.

“Leo Magufuli najua ameapa na kuilinda Katiba,itashangaza kuona Kesho Dk Shein kama ataingia kwenye Bunge wakati ni ukweli kwamba katiba ya Zanzibar inaonyesha wazi ameshamaliza muda wake wa uongozi kwa kipindi cha miaka mitano,sasa kama kesho akiwepo kitendo hiko hakitakubalika na kinafaa kupingwa ka kila Mtanzania”,amesema Profesa Lipumba.

Kuibuka huko kwa Profesa Lipumba kunakuja ikiwa ni siku moja kupita baada ya Wabunge wanaounda muungano wa Vyama vya Ukawa,kumwandikia Barua Spika wa Bunge wa Job Ndugai na kutaka uhalali wa Rais Magufuli kuhutubia Bunge wakati Zanzibar bado hawajapata Rais wake.
 
Akisoma Barua hiyo jana Mjini Dodoma kwa niaba ya Wenzake mwenyekiti mwenza wa Umoja huo,Freeman Mbowe amesema Wabunge wa Ukawa hawatakakubali katika mazingira yeyote kuruhusu katiba ya nchi ambayo imetokana na matakwa ya wananchi ikuvunjwa hadharani.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo hai amesema njia pekee watakayotumia mwaka huu si ile waliyotumia mwaka 2010 kumsusia Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwa kutoka nje huku wakidai njia watakayoitumia sasa hivi ni kupambana ndani ya Bunge mpaka haki itakapopatikana.

Pia wameficha njia watakayotumia kwa kuwataka wanahabari wasubiri siku hiyo ifike. 
Via>>Udakuspecially.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com