ANGALIA PICHA NA VIDEO- RAIS MAGUFULI ALIPOFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA HOSPITALI YA MUHIMBILI..AKUTANA NA MADUDU YA HATARI


Rais John Magufuli leo amefanya ziara ya ghafla katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa lengo la kujionea uhalisia wa huduma inayotolewa.

Kama ilivyokuwa alipofanya ziara ya kushtukiza katika Wizara ya Fedha wiki iliyopita, Rais Magufuli alikutana na viongozi wa hospitali hiyo na kuongozana nao katika maeneo ambayo aliyachagua yeye.


Rais amesikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini.

Pia amekasirishwa na hali ya kutokujali wala kushughulikia vifaa vya kufanyia kazi ambapo amekuta mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN zikiwa hazifanyi kazi kwa muda wa miezi miwili sasa, ilihali mashine kama hizo katika Hospitali za binafsi zinafanya kazi na wagonjwa wanaelekezwa kwenda kutafuta huduma huko







Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post