Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Angalia Picha 10!! HAYA NDIYO MAJANGA YA KRISMASI SHINYANGA,BARABARA MBOVU YASABABISHA AJALI



Jafari Ramadhani(20) mkazi wa mtaa wa Bugweto kata ya Ibadakuli katika manispaa ya Shinyanga akiwa eneo la tukio baada ya pikipiki aliyokuwa anaendesha kugongana uso kwa uso na gari ndogo katika barabara ya Mohammed Trans karibu na shule ya msingi Bugoyi B.Licha ya kugongana na pikipiki hiyo,pia mwendesha baiskeli aliyejulikana kwa jina la Peter Machanga amenusurika kufa baada ya kuruka na kuacha baiskeli ikagongwa na gari hilo.Tukio hilo limetokea leo majira ya saa nne asubuhi.Kwa mujibu wa mashuhuda wanasema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva wa gari pamoja ubovu wa barabara hiyo ambayo ina mashimo mengi-Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog





Pikipiki yenye namba za usajiri T 142 BAN aina Luhao iliyokuwa inaendeshwa na Jafari Ramadhan alivunjika mguu wake wa kushoto na kuumia sehemu mbalimbali za mwili wake




Gari Toyota lenye namba za usajiri T 816 BEH aina ya Toyota Sprinter lililosababisha mwendesha pikipiki Jafari Ramadhani amalizie kusherehekea sikukuu ya Krismasi Vibaya



Mashuhuda wa tukio hilo wanasema Jafari Ramadhan alikuwa anaendesha pikipiki yenye namba za usajiri T 142 BAN aina Luhao katika barabara hiyo ambapo ghafla aligongana uso kwa uso na gari hiyo kisha gari kugonga baiskeli iliyokuwa inaendeshwa na Peter Machanga aliyeruka baada ya kuona hatari hiyo.





Mashuhuda wanasema ajali hiyo imechangiwa kwa kiasi kikubwa na ubovu wa barabara hiyo kwani ina mashimo mengi hali iliyosababisha mwendesha gari,pikipiki na baiskeli wakijikute wakiwa sehemu moja huku wananchi waishio karibu na barabara hiyo wameiambia Malunde1 blog kuwa ndani ya wiki moja pekee watu zaidi ya watano wagongwa na magari na pikipiki kutokana na ubovu wa barabara hiyo ya vumbi inayotumiwa na wakazi wa mjini Shinyanga




Muonekano wa nyuma wa gari hiyo




Mashuhuda wa tukio wakitoa maelezo kwa askari wa usalama barabarani ambapo walisema ndani ya gari hilo kulikuwa na vijana wawili ambao walikimbia baada ya kutokea ajali hiyo kukwepa kichapo kutoka kwa wananchi na baadaye kuokolewa na msamaria mwema aliyekuwa na gari aliyeamua kuwapandisha kwenye gari lake kisha kuwapeleka katika kituo cha polisi




Wananchi wakiwa eneo la tukio




Askari wa usalama barabarani akiwa eneo la tukio




Wananchi wakiondoa gari kwenye mtaro..Akizungumza na mtandao huu akiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga anakopatiwa matibabu Jafari Ramadhani amesema gari hiyo ilikuwa katika mwendo kasi ikikwepa mashimo,na kilichomfanya asiumie zaidi ni kofia ngumu(helment) aliyokuwa amevaa-Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com