Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Angalia picha 15!! KIKAO CHA TAWLAE NA WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA,MWANDISHI WA MAJIRA ANG'AA TUZO YA HABARI ZA WAZEE MWAKA 2015



 
Hapa ni katika ukumbi wa Mwalimu House mjini Shinyanga,pichani ni katibu wa asasi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Association of Woman Leaders in Agriculture and Environment(TAWLAE),inayojihusisha na haki za wazee tawi la Shinyanga Hellen Maleza akizungumza jana katika kikao cha TAWLAE na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.
Lengo la kikao hicho cha siku moja ni kuhamasisha waandishi wa habari juu ya umuhimu wao katika kuhamasisha jamii na viongozi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu wazee.
 
Pamoja na mambo mengine Shirika lisilo la kiserikali la HelpAge International linalojihusisha na utetezi wa haki za wazee linalofanya kazi na TAWLAE limempa tuzo ya uandishi bora wa habari za wazee nchini mwandishi wa habari wa gazeti la Majira Suleiman Abeid kwa kumpatia kitita cha shilingi 200,000/=.Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog




Kikao kinaendelea,ambapo waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga walipanga mikakati mbalimbali ya kushughulika na mambo ya wazee katika jamii




Mwandishi wa habari gazeti la Uhuru na Mzalendo Chibura Makorongo akiwa ukumbini




Katibu wa asasi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Association of Woman Leaders in Agriculture and Environment(TAWLAE),inayojihusisha na haki za wazee tawi la Shinyanga Hellen Maleza akizungumza katika kikao hicho




Kikao kinaendelea




Wadau wa haki za wazee wakiwa ukumbini




Kikao kinaendelea




Kikao kinaendelea




Katibu wa asasi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Association of Woman Leaders in Agriculture and Environment(TAWLAE)tawi la Shinyanga Hellen Maleza akionesha moja ya makala kuhusu wazee iliyoandikwa na mwandishi wa habari wa gazeti la Majira Suleiman Abeid ikiwa ni miongoni mwa makala 20 alizoandika kuanzia mwaka 2013 hadi 2015 na kufanikiwa kumpa ushindi wa tuzo ya mwandishi bora wa habari kuhusu wazee nchini Tanzania





Kushoto ni mwenyekiti wa Baraza la Wazee mkoa wa Shinyanga Selina Mkula kutoka Kahama akikabidhi tuzo ya shilingi 200,000/- kwa mwandishi bora wa habari za wazee nchini Tanzania mwaka 2015,Suleiman Abeid wa gazeti la Majira,zilizotolewa na shirika la HelpAge International linalohusika na utetezi wa haki za wazee.




Mwandishi wa habari Suleiman Abeid akishikana mkono na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee mkoa wa Shinyanga Selina Mkula baada ya kupokea pesa taslimu shilingi laki mbili






Kushoto ni katibu wa asasi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Association of Woman Leaders in Agriculture and Environment(TAWLAE) Hellen Maleza akishikana mkono na mshindi wa tuzo ya uandishi wa habari za wazee 2015,Suleiman Abeid





Kulia ni mwandishi wa habari Suleiman Abeid akionesha kitita cha shilingi laki 2 alizopewa baada ya kuibuka mshindi tuzo ya uandishi bora wa habari za wazee



Picha ya pamoja,wa pili kutoka kulia ni mwenyekiti wa kikao cha TAWLAE na waandishi wa habari Sam Bahari,mwandishi wa gazeti la Mtanzania




Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com