Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Angalia Picha 37!! UZINDUZI WA KAMPENI YA KUHAMASISHA MATUMIZI YA MAFUTA YA ALIZETI YALIYOONGEZWA VITAMINI A KATIKA MANISPAA YA SHINYANGA



Hapa ni katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga ambako leo Desemba 04,2015 kumefanyika uzinduzi wa mradi wa kuhamasisha Matumizi ya Mafuta ya Kupikia ya Alizeti yaliyoongezwa Vitamini A. Mradi huo/kampeni hiyo ya Kuhamasisha matumizi ya Mafuta ya Alizeti  yenye Vitamini A imeandaliwa na shirika la Tanzania Communication and Development Center(TCDC) kushirikiana  shirika la Menonite Economic Development Association(MEDA) umezinduliwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga.TCDC wanajihusisha na mambo ya uhamasishaji wa jamii kuhusu afya na lishe-Malunde1 blog ilikuwepo eneo la tukio...Mwandishi wetu Kadama Malunde ametuletea picha 36 kilichojiri..angalia hapa chini


Mafuta ya alizeti yenye ujazo wa lita 1,yanayotengenezwa mkoani Singida na Manyara ambayo sasa yanauzwa kwa bei ya punguzo shilingi 2900 badala ya shilingi 3800...Unachotakiwa kufanya ni >>Andika neno MA kwenda namba 15027 ,utapokea Ujumbe kutoka Media,kisha utaonesha ujumbe huo kwa muuzaji aliyesajiliwa kuuza mafuta ya alizeti yaliyoongezwa Vitamini A...Kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0685-444282 au www.masava.org
Katikati ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akiwa katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha matumizi ya Mafuta ya alizeti yaliyoongezwa Vitamin A


Meza kuu

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akielekea katika banda la Mawakala wanaouza mafuta hayo


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akisalimiana na mawakala wa mafuta ya alizeti

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akiangalia mafuta hayo,kushoto ni Meneja wa shirika la Tanzania Communication and Development Center(TCDC) mkoa wa Shinyanga na Mwanza Mgalula Mathias Ginai akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa kuhusu mafuta ya alizeti yaliyoongezwa virutubisho vya vitamini A

Wadau wa mafuta ya alizeti wakiwa eneo la tukio
Vitamini A inasaidia mambo makuu matano katika mwili wa binadamu,ambayo ni kusaidia macho kuona hasa kwenye mwanga hafifu,kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa,ukuaji bora kwa mtoto,kuimarisha mfumo wa uzazi kwa wanawake na wanaume na kufanya ngozi kuwa nyororo

Wachezaji wa ngoma ya asili ya Ununguli wakitoa burudani

Mchezaji wa Ngoma ya Ununguli akitoa nyoka kwa mdomo kutoka kwenye sanduku



Jamaa anacheza na nyoka


Jamaa anacheza na nyoka



Meneja wa shirika la Tanzania Communication and Development Center(TCDC) mkoa wa Shinyanga na Mwanza Mgalula Mathias Ginai akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo,ambapo alisema wataendelea na kampeni hiyo kwa muda wa siku 5 katika halmashauri tatu za mkoa wa Shinyanga ambazo ni manispaa ya Shinyanga,halmashauri ya Shinyanga na halmashauri ya mji Kahama.



Msanii Chapchap na wanenguaji wake wakitoa burudani..nyuma yao ni Jukwaa la MC Ice anayepatikana mjini Shinyanga


Watoto wajiandaa kutoa burudani,nyuma yao ni MC Ice akiwa katika Jukwaa ambalo kama unahitaji kulitumia kwa shughuli yoyote unawasiliana nae kwa simu namba 0757988526





Afisa Lishe wa mkoa wa Shinyanga Dk Mwita Chacha Ngutunyi akizungumza wakati wa uzinduzi huo

Mwakilishi wa shirika la Menonite Economic Development Association(MEDA) Emmanuel Peter akizungumza wakati wa uzinduzi huo

Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi huo

Mgeni rasmi ,mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambapo alisema mafuta hayo yatasaidia kupunguza tatizo na utapiamlo na udumavu wa watoto mkoani Shinyanga


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akikata utepe kuashiria kufungua rasmi kwa kampeni ya kuhamasisha matumizi ya mafuta ya alizeti yaliyoongezwa Vitamini A


Burudani ikachukua nafasi yake..vijana wa Shinyanga wakicheza

Wanafunzi nao walikuwepo

Tunafuatilia kinachoendelea hapa

Vijana wakionesha vipaji vyao vya kucheza

Msanii maarufu kwa Jina la Chapchap akitoa burudani

Mc maarufu nchini Tanzania anayejuliana kwa jina la ICE akifanya yake

Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio


Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio

Tunafuatilia kinachojiri hapa..

Watoto nao wamo...wanacheza balaa

Tunaangalia burudani

Kulia ni msanii Chapchap,katika wakala wa Mafuta ya alizeti na Mc ICE wakielezea umuhimu wa mafuta ya alizeto yaliyoongezwa Vitamini A



Picha ya kumbukumbu na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga,kila mmoja kashikilia chupa ya mafuta ya alizeti




Picha ya pamoja

Picha ya kumbukumbu

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

BOFYA HAPA UANGALIE PICHA 42 ZA UZINDUZI WA MRADI WA MAFUTA YA ALIZETI YENYE VITAMINI A HUKO KAHAMA 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com