Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA 60 ZA MKUTANO WA KWANZA WA BARAZA LA MADIWANI WA MANISPAA YA SHINYANGA,MADIWANI WAAPISHWA NA MEYA ACHAGULIWA


Hapa ni katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambapo mkutano wa kwanza wa baraza la madiwani wa manispaa ya Shinyanga umefanyika leo Alhamis Desemba 10,2015.Pamoja na mambo mengine madiwani wamekula kiapo cha uaminifu na kufanya uchaguzi wa meya na naibu meya wa manispaa hiyo.Mwandishi wetu Kadama Malunde ametuletea picha 60 za matukio yaliyojiri katika eneo la tukio..Angalia hapa chini




Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna akiwakaribisha wajumbe wa mkutano huo wa kwanza wa baraza la madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga



Mwenyekiti wa muda wa baraza la mdiwani wa manispaa ya Shinyanga Charles Maugira akizungumza katika baraza hilo la madiwani



Madiwani wa manispaa ya Shinyanga kabla ya kula kiapo cha uaminifu wakiwa ukumbini



Wakuu wa idara katika manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini



Sekretariati ya baraza la madiwani



Madiwani wa Chama Cha Mapinduzi kabla ya kula kiapo cha uaminifu



Madiwani wa Chadema kabla ya kula kiapo cha uaminifu



Madiwani wa CCM wakiwa ukumbini



Wajumbe wa mkutano huo wakiwa ukumbini



Wageni waalikwa wakiwa ukumbini



Mkutano unaendelea



Diwani wa viti maalum kupitia Chadema,Zainabu Heri akiwa ukumbini



Madiwani wa Chadema wakiwa ukumbini



Madiwani wa CCM wakiwa ukumbini kabla ya kula kiapo



Mkutano unaendelea



Mkutano unaendelea



Wafanya kazi wa manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini



Mkutano unaendelea



Maafisa kutoka manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini



Mkutano unaendelea



Maafisa kutoka manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini



Wageni waalikwa wakiwa ukumbini



Mkutano unaendelea



Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Shinyanga wakiwa ukumbini



Wageni waalikwa wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini



Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Charles Sangura akifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika baraza hilo



Hakimu mkazi wilaya ya Shinyanga Lydia Ilunda akitoa maelekezo kwa madiwani wa manispaa ya Shinyanga kabla ya kuanza kuwaapisha katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga



Wageni waalikwa wakiwa ukumbini



Madiwani wa manispaa ya Shinyanga wakivaa majoho tayari kwa kula kiapo cha uaminifu



Madiwani wakila kiapo cha uaminifu




Hakimu mkazi wilaya ya Shinyanga Lydia Ilunda akiapisha madiwani wa manispaa ya Shinyanga



Madiwani wakila kiapo



Madiwani wakila kiapo



Madiwani wakila kiapo



Madiwani wakiendelea kula kiapo



Nakula kiapo cha uaminifu.....



Madiwani wakila kiapo cha uaminifu



Tunakula kiapo



Tunafuatilia kinachoendelea humu ndani



Madiwani wakijaza fomu za kiapo



Tunajaza fomu za kiapo



Najaza fomu ya kiapo



Hakimu mkazi wilaya ya Shinyanga Lydia Ilunda akisisitiza jambo baada ya madiwani kula kiapo cha uaminifu



Hakimu mkazi wilaya ya Shinyanga Lydia Ilunda akizungumza baada ya madiwani kumaliza kula kiapo cha uaminifu





Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna akitoa muongozo kuhusu uchaguzi wa meya na naibu meya wa manispaa ya Shinyanga ambapo aliwataja waliojitokeza kugombea nafasi ya udiwani kuwa ni diwani wa kata ya Shinyanga mjini Gulam Hafeez Mukadam(CCM) na Emmanuel Ntobi,ambaye ni diwani wa kata ya Ngokolo(Chadema).Waliojitokeza kugombea nafasi ya unaibu meya ni Agnes Machiya diwani wa kata ya Kolandoto na Samwel Sambayi (Chadema)




Msimamizi wa uchaguzi wa meya na naibu meya wa manispaa ya Shinyanga,Charles Maugira akiwaita wagombea wa nafasi hizo waombe kura kwa wapira kura 23.



Diwani wa kata ya Ngokolo Emmanuel Ntobi (CHADEMA)akiomba kura ili achaguliwe kuwa meya wa manispaa ya Shinyanga



Diwani wa kata ya Shinyanga Mjini Gulam Hafeez Mukadam akiomba kura ili achaguliwe kuwa meya wa manispaa ya Shinyanga kwa awamu ya pili



Mgombea nafasi ya unaibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya



Mgombea unaibu meya manispaa ya Shinyanga kupitia CHADEMA, Samwel Sambayi akiomba kura




Mkurugenzi wa manipaa ya Shinyang Lewis Kalinjuna akimpongeza diwani wa kata ya Shinyanga mjini Gulam Hafeez Mukadam aliyekuwa anagombea nafasi ya meya kwa awamu ya pili.Msimamizi wa uchaguzi huo, Charles Maugira alimtangaza Mukadam kuwa Mstahiki Meya baada ya kupata kura 16 na kumshinda mpinzani wake kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Emmanuel Ntobi aliyepata kura saba.Nafasi ya Unaibu meya, mgombea wa CCM, Agnes Machiya alipata kura 16 huku mgombea wa CHADEMA, Samwel Sambayi akiambulia kura saba.



Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam(katikatiO na naibu meya Agnes Machiya wakivaa majoho ya nafasi hizo,kushoto ni mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna naye anavaa jopo




Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akiwashuru madiwani wa manispaa ya Shinyanga kwa kumchagua kwa awamu ya pili kuongoza miaka mitano ambapo ameahidi kushirikiana na madiwani wa vyama vyote ili kuwaletea maendeleo wananchi



Meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez akiendesha baraza la madiwani baada ya uchaguzi wa nafasi ya meya na naibu meya...

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza wakati wa mkutano wa kwanza wa baraza la madiwani wa manispaa ya Shinyanga ambapo amewataka madiwani wote kuungana bila kujali itikadi za kichama katika kuwaletea maendeleo wananchi badala ya kuendekeza malumbano



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amewataka madiwani hao kufanya kazi kwa kufuata kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano chini ya rais John Pombe Magufuli ya Hapa Kazi tu huku akiwasisitiza madiwani kuwa wabunifu ili kuwaletea maendeleo wananchi.Katika hatua nyingine amewataka madiwani kuhamasisha suala la usafi katika maeneo yao ikiwemo ujenzi wa vyoo kwani amebaini kuwa kaya nyingi katika wilaya ya Shinyanga hazina vyoo.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com