Hapa ni katika viwanja vya CDT vilivyopo mjini Kahama mkoani Shinyanga ambapo leo Jumapili Desemba 06,2015 kumefanyika uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha matumizi ya mafuta ya alizeti yaliyoongezwa virutubisho vya Vitamini A.Mgeni rasmi alikuwa kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya mji Kahama Michael Mzengula ambaye ni afisa kilimo wa manispaa hiyo.
Kampeni hiyo imeandaliwa na shirika la Tanzania Communication and Development Center(TCDC) wakishirikiana na shirika la Menonite Economic Development Association(MEDA) na shirika la Ushauri na Udhibiti wa Ukimwi Kahama (SHIUUKA).
Mradi huu wa mafuta ya asili ya alizeti yenye vitamini A umeanzia katika mikoa ya Manyara na Shinyanga baada ya utafiti kuonesha kuwa mikoa hiyo ina tatizo la upungufu mkubwa wa Vitamini A kwa watoto na akina mama.Kutoka Kahama mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha 42 za matukio yote yaliyojiri wakati wa uzinduzi huo..Tazama hapa chini.
Baadhi ya maafisa kutoka shirika TCDC na shirika The Voice of Marginalized Community(TVMC )pamoja na wakazi wa Kahama wakiwa eneo la tukio
Wakazi wa Kahama wakiwa eneo la tukio.Mafuta na ya alizeti yaliyoongezwa Vitamini A yanazalishwa katika mkoa wa Manyara katika kiwanda cha Shams Muktar na kiwanda cha Sunshine na Sweet Drop mkoani Singida na mafuta hayo yanapatikana kwa mawakala wanaopatikana katika kila kata mbalimbali.
Waigizaji kutoka kundi la sanaa za maonesho kinachojulikana kwa jina la Kahama Medical Culture Troup(KMC) wakitoa ujumbe kwa njia ya igizo kuhusu umuhimu wa mafuta ya asili ya alizeti yaliyoongezwa virutubisho vya Vitamini A.
Wakazi wa Kahama wakiwa eneo la tukio
Waigizaji kutoka KMC wakitoa burudani
Watoto wa Kahama wakicheza muziki...hawa watoto sijui huwa wanajifunzia wapi kukata viuno...Mh ni hatari sana...
Msanii Nyanda Kawa kutoka kundi la sanaa za maonesho kinachojulikana kwa jina la Kahama Medical Culture Troup(KMC) akicheza ngoma ya asili
Mkazi wa Kahama akiwa amebeba mtoto akifuatilia kilichokuwa kinaendelea wakati wa uzinduzi huo ambapo miongoni mwa faida za vitamini A ni kusaidia ukuaji bora na maendeleo ya mtoto.
Msanii Nyanda Kawa kutoka kundi la sanaa za maonesho kinachojulikana kwa jina la Kahama Medical Culture Troup(KMC) akiwa na mwenzake wakitoa nyoka aina ya Chatu
Msanii Nyanda Kawa akimwingiza nyoka aina ya chatu katika sehemu zake za siri
Msanii Nyanda Kawa kutoka kundi la sanaa za maonesho kinachojulikana kwa jina la Kahama Medical Culture Troup(KMC) akicheza na nyoka aina ya Chatu.
Meneja wa shirika la Tanzania Communication and Development Center(TCDC) mkoa wa Shinyanga na Mwanza Mgalula Mathias Ginai(mbele) akaamua kupiga picha ya kumbukumbu na Msanii Nyanda Kawa kutoka kundi la sanaa za maonesho kinachojulikana kwa jina la Kahama Medical Culture Troup(KMC) aliyevuta hisia za wakazi wa Kahama kwa kucheza na nyoka bila uoga wowote.
Kushoto mwenye nguo nyeusi ni mkurugenzi wa shirika The Voice of Marginalized Community(TVMC ) lenye makao makuu yake mkoani Shinyanga Musa Jonas Ngangala akifuatiwa na mkurugenzi wa Malunde1 blog yenye makao yake makuu mkoani Shinyanga Kadama Malunde wakiwa katika picha ya pamoja na Msanii Nyanda Kawa kutoka kundi la sanaa za maonesho kinachojulikana kwa jina la Kahama Medical Culture Troup(KMC)
Tunapiga picha ya kumbukumbu…..Picha Chwaaa!!
Msanii mwenye fani nyingi maarufu kwa jina la CHAPCHAP akitoa burudani katika viwanja vya CDT mjini Kahama,msanii huyo mwenye makazi yake mkoani Shinyanga huwa anaimba nyimbo za kiutamaduni,dansi,vichekesho na maigizo na mara kwa mara amekuwa akifanya kazi na shirika The Voice of Marginalized Community(TVMC ).
Msanii CHAPCHAP akitoa ujumbe kwa hisia kuhusu umuhimu wa Vitamini A katika mwili wa binadamu.
Kulia ni mkurugenzi wa shirika The Voice of Marginalized Community(TVMC ) Musa Jonas Ngangala akicheza na msanii Chapchap.
Afisa mradi kutoka shirika la ushauri na udhibiti wa Ukimwi Kahama Deogratias Machimu akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha matumizi ya mafuta ya alizeti yenye Vitamini A ambapo alisema kutokana na utafiti uliofanywa na shirika la MEDA upungufu wa vitamini A nchini Tanzania unaathiri kwa kiwango cha kati ya watoto wenye umri kati ya miezi 6 hadi 59 kwa asilimia 34 na kina mama wenye uuwezo wa kujifungua kati ya umri wa miaka 15 hadi 49 kwa asilimia 37 na mkoa unaoongoza kwa upungufu mkubwa wa Vitamini A ni Shinyanga na Manyara.
Mkurugenzi wa shirika The Voice of Marginalized Community(TVMC ) Musa Jonas Ngangala akihudumia wakazi wa Kahama waliohudhuria shughuli ya uzinduzi huo baada ya kutambua umuhimu wa mafuta ya alizeti yenye vitamini A na kuamua kununua.
Mkurugenzi wa shirika The Voice of Marginalized Community(TVMC ) Musa Jonas Ngangala akitoa elimu kwa wakazi wa Kahama juu ya umuhimu wa mafuta hayo yanayosaidia macho kuona vizuri hasa katika mwanga hafifu na kuimarisha mfumo wa uzazi kwa wanawake na wanaume sambamba na kufanya ngozi kuwa nyororo.
Mkurugenzi wa shirika The Voice of Marginalized Community(TVMC ) Musa Jonas Ngangala akipokea pesa baada ya mkazi wa Kahama kununua mafuta ya alizeti yenye vitamini A.
Mkurugenzi wa shirika The Voice of Marginalized Community(TVMC ) Musa Jonas Ngangala akifafanua juu ya umuhimu wa mafuta hayo ambayo yanaimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa.
Meneja wa shirika la Tanzania Communication and Development Center(TCDC) mkoa wa Shinyanga na Mwanza Mgalula Mathias Ginai akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ambapo alisema wameanzisha mradi huo ili kuhakikisha kuwa jamii inakuwa na afya bora hivyo kuwataka wadau wote kushirikiana katika kufanikisha mradi huo.
Meneja wa shirika la Tanzania Communication and Development Center(TCDC) mkoa wa Shinyanga na Mwanza Mgalula Mathias Ginai akiwahamasisha wakazi wa Kahama kununua mafuta ya alizeti yenye virutubisho vya Vitamini kwani yana faida nyingi katika mwili wa binadamu.
Vijana wa Hamasa wakitoa burudani
Afisa Lishe halmashauri ya mji Kahama Mwanaidi Lukali akizungumza wakati wa uzinduzi huo
Afisa mradi kutoka shirika la ushauri na udhibiti wa Ukimwi Kahama Deogratias Machimu akionesha mfano wa Bango atakalokuwa nalo wakala wa mafuta ya alizeti yenye Vitamini A kila kata wilayani Kahama.
Mgeni rasmi mkurugenzi wa halmashauri ya mji Kahama Michael Mzengula akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambapo alisisitiza umuhimu wa mafuta hayo.
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Tunafuatilia kinachojiri hapa
Wakazi wa Kahama wakiwa eneo la tukio
Msanii Chapchap kutoka Shinyanga akiimba wimbo kabla ya kuanza kuvua chupi zaidi ya 30 alizokuwa amevaa ikiwa ni sehemu ya vituko na vichekesho vyake…
Msanii Chapchap akivua chupi moja baada ya nyingine…Ni vituko balaa
Msanii Chap Chap akionesha mbwembwe zake
Msanii Chapchap akichekesha….
DJ Maarufu mkoani Shinyanga Salum Mawazo maarufu kwa jina la DJ Salu kutoka BIG 5 Promotion Sound wanaopatikana mjini Shinyanga akiwa ndani ya Gari lao la Matangazo akifanya yake katika viwanja vya CDT mjini Kahama.
Je Unafahamu umuhimu wa Vitamini A mwilini??? Ni Msanii Chap Chap akimuuliza maswali Adam Mwihechi meneja wa BIG 5 Promotion Sound ambao wanatoa huduma ya Gym ,vifaa vya muziki,wana gari la Matangazo kwa ajili ya Public Announcement(PA).
Mkurugenzi wa shirika The Voice of Marginalized Community(TVMC ) lenye makao makuu yake mkoani Shinyanga Musa Jonas Ngangala akitoa maelezo kwa wafanyabiashara mjini Kahama waliotaka kuwa mawakala wa kuuza mafuta ya alizeti yaliyoongezwa vitamini A
Msanii Chapchap akionesha bango atakalokuwa nalo wakala wa kuuza mafuta ya alizeti yenye Vitamini A
MC Maarufu nchini Tanzani,ICE akiwa na wakazi wa Kahama mjini akiendesha mchezo wa kurushiana Tisheti kisha kutoa zawadi ya tisheti kwa mshindi..
MC ICE (katikati) akigawa tisheti kwa wakazi wa Kahama zenye nembo ya mafuta ya alizeti yenye Vitamini A
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog
BONYEZA MANENO HAYA KUANGALIA PICHA 37 ZA UZINDUZI WA KAMPENI YA KUHAMASISHA MATUMIZI YA MAFUTA YA ALIZETI YALIYOONGEZWA VITAMINI A KATIKA MANISPAA YA SHINYANGA
Social Plugin