Zaidi ya kaya 250 za bonde la Mkwajuni jijini Dar es Salaam hazina makazi ya kuishi kutokana na zoezi la bomoabomoa linaloendelea ambapo wameiomba serikali kuwatafutia mahali mbadala pa kuishi kwani hawana njia nyingine mbadala ya kujiondoa katika dhahama hiyo.
Mwandishi wa habari hizi alifika katika eneo hilo na kushuhudia makundi mbalimbali ya wananchi wakiwa hawaamini kinachoendelea kutoka na jinsi tinga tinga linavyoshusha nyumba hizo chini huku ulinzi wa jeshi la polisi ukiwa umeimarishwa.
Baadhi ya wahanga wa bomoabomoa hiyo wamesema hawana pakwenda na jambo kubwa ni serikali iwatafutie sehemu nyingine ya kuishi kwani zoezi limekuwa la ghafla sana.
Katika kuonyesha kuwa kweli wahanga hao hawana sehemu mbadala ya kwenda baadhi ya watu waliobomoloewa nyumba zao siku ya kwanza bado wanaishi katika eneo hilo pamoja na watoto.
Wakizungumzia zoezi hilo afisa mipango miji Dk Charles Mkalawa kutoka wizarani na mwanasheria wa NEMC Bw Mancari Heche Suguta wamesema mpaka sasa hivi zaidi ya nyumba 150 zimebomolewa na zoezi linaendelea..
Via>>ITV
Social Plugin