BASI LA ALLY'S LAUA WATU NANE HUKO TABORA,MAJERUHI ZAIDI YA 10
Tuesday, December 15, 2015
Watu wanane wamefariki dunia papo hapo na wengine 14 katika ajali mbaya eneo la kijiji cha Vumilia wilayani Urambo mkoani Tabora. iliyohusisha basi la kampuni ya ALLY'S lililokuwa likitokea wilayani Kaliua kuelekea jijini Mwanza, baada ya kuteleza na kupinduka kutokana na mwendo wa kasi katika mvua zinazoendelea kunyesha mkoani humo. Akitoa taarifa za tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Tabora kamishina msaidizi Hamis Suleimani, amesema gali hilo lenye namba za usajili T 143 CQT lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina la Alfa Haji ambaye alitoroka baada ya kusababisha ajali hiyo, na jeshi la polisi linaendelea kumtafuta, ili ajibu tuhuma zinazo mkabili.
Aidha kamanda wa polisi Hamis Suleimani amewataka madereva wote mkoani Tabora kuwa makini na ajali kwa kwenda mwendo wa kawaida ili kuwanusuru ambiria kwani wanaposababisha ajali wanaliongezea taifa gharama zisizo za msingi za kuwahudumia na kwa gharama ambazo zingefanya shuguli nyingine.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin