Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAJAMBAZI TENA SHINYANGA....YAVAMIA DUKA LA MPESA KAMBARAGE,YAPORA NA KUJERUHI WATU WATATU



Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba watu zaidi ya wawili wanaodaiwa kuwa ni majambazi wamevamia duka la Mpesa lililopo eneo la Soko la Kambarage karibu na dampo la taka ama Magunya Stationary mjini Shinyanga kisha kujeruhi watu watatu kwa risasi na kupora pesa zinazodaiwa kuwa shilingi milioni 6.


 Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa tukio hilo limetokea usiku huu majira ya saa mbili,ambapo watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi walifika katika duka hilo kisha kurusha risasi hewani,kumjeruhi binti aliyekuwa akitoa huduma ya MPESA katika duka hilo na watu wengine wawili waliokuwa eneo hilo.

Inaelezwa kuwa mbali na kupora pesa pia wameondoka na vitu mbalimbali zikiwemo simu za mkononi.

SOMA TAARIFA KAMILI HAPA

Tukio la majambazi kuvamia duka la MPESA limekuja wiki moja tu baada ya majambazi kuvamia duka katika stendi ya mabasi yaendayo mikoani,ambapo pia walijeruhi watu wawili kisha kupora simu,vocha za simu na pesa vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 5.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com