Habari tulizozipata hivi punde katika chumba cha habari cha Malunde1 blog ni kwamba watu watatu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wanaodaiwa kuwa walikuwa wamevaa kama polisi wamevamia katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani mjini Shinyanga maarufu kwa jina la Stendi ya Manyoni.
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema majambazi hayo yamevamia duka la mfanyabiashara anayejulikana kwa jina la Mwita majira ya saa mbili usiku leo Desemba 02,2015.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo anasema majambazi hayo baada ya kufika katika duka hilo yalifyatua risasi hewani kisha kuingia ndani ya duka na kuwaamuru waliokuwa ndani kulala chini lakini kijana mmoja ambaye hufanya kazi ya kuchoma nyimbo katika stendi hiyo hakulala,akapigwa risasi ya mguuni.
Taarifa za awali zinasema kuwa majambazi hao wamefanikiwa kupora pesa zinazodaiwa kuwa shilingi milioni tano na kutokomea kusikojulikana.
SOMA HABARI KAMILI <<HAPA>>
Social Plugin