DEREVA ALIYESABABISHA AJALI ILIYOUA WATU 12 HUKO SINGIDA AKAMATWA NA POLISI


Jeshi la Polisi mkoani Singida limefanikiwa kumkamata dereva aliyesababisha ajali ya basi la Takbiri lililokuwa likitoka Dar-es-Salaam na kuelekea Geita kugongana na maroli mawili na kusababisha vifo vya watu kumina mbili katika barabara kuu ya Singida Mwanza ambayo ime tokea katika kijiji cha Kizonzo wilayani Iramba.

Akiongea kwa njia ya simu akiwa katika eneo la ajali kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Singida ACP Thobias Sedoyeka amesema dereva huyo aliyetambulika kwa jina la Charles Kapema ambaye amekiri kosa kwa kusababisha ajali kwa uzembe amekamatwa wilayani Igunga na kusema kuwa aliamua kukimbia kwa kuhofia usalama wake.

Akiongea kwa shida huku akiwa amelazwa, Bi.Roda Mbata ambaye maarufu kwa jina la mama mchungaji Preje ni mmoja wa majeruhi pamoja na kusema dereva alikuwa akiendesha basi kwa mwendo wa kasi, ameliomba jeshi la Polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kushirikiana na serekali kupiga marufuku mabasi kusafiri usiku kwani madereva wengi wametumia mwanya huo kukimbiaza mabasi pindi askari wa usalama barabarani wanapo kuwa hawapo.

Katika hatua nyingine kamanda Sedo Yeka amejibu swali la abiria aliyeomba mabasi ifikapo saa kumina mbili kusitisha safari na kulala, amekiri kuwa madereva wa mabasi wengi inapofika saa kumina mbili wakati askari hawapo huwa wana kimbiza sana mabasi, kwahiyo atahakikisha ombi hilo analifikisha katika ngazi husika ili lifanyiwe kazi.

Kwa upande wake katibu wa hospitali ya wilaya ya Iramba Bwana Kalen Ngungu akiongea na mwandishi wa habari hizi kwa simu kuhusu rufaa kwa majeruhi, waliobaki kutibiwa na maiti ambazo zimekosa majokofu ya kuhifadhia, alikuwa na haya ya kusema.

Ajali hiyo ambayo imetokea 01.12.2015 majira ya saa tatu usiku katika kijiji cha Kizonzo mpakani na wilaya ya Igunga na wilaya ya Iramba, dereva wa basi hilo awali alitozwa faini mkoani Singida kwa kuendesha basi kwa mwendo wa kasi, lakini adhabu hiyo haikuwa fundisho badala yake aliendelea na mwendo kasi na kusababisha ajali, vifoo na majeruhi bila sababu yoyote.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post