Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Duh!! KIMBUNGA CHA MAGUFULI CHAWAKUMBA HADI OMBA OMBA WA DAR!! NAO WANAONDOLEWA MKUU WA MKOA ADAI WANACHANGIA UCHAFU



MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri za jiji la Dar es Salaam, kuwaondoa ombaomba wote walioko katika barabara za jiji, kwani wanachangia uchafu.



Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Sadiki alisema utekelezaji wa kauli ya Rais John Magufuli ya kutumia siku ya Desemba 9 mwaka huu kufanya usafi, utakwenda sambamba na kuwaondoa ombaomba hao, ambao wanachangia kuongeza uchafu.

“Siwezi kusema wao ni uchafu lakini mazingira yanayowazunguka katika maeneo wanayofanyia shughuli zao wanayachafua, wanajisaidia kwenye mifuko na kutupa ovyo,” alisema.

Alisema viongozi ambao wako katika maeneo ambayo ombaomba hao wanarudi, wahakikishe hawarudi mjini kwa sababu imekuwa ni tabia ya omba omba hao wanaporudishwa baada ya muda kurudi tena jijini.

Aidha, aliiagiza Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kushirikiana na Jeshi la Polisi kuwaondoa wapigadebe katika vituo vya daladala kwani wamekuwa kero kwa abiria. 


Chanzo-Mpekuzi blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com