JESHI LA POLISI LINAWASAKA WALIOENEZA MTANDAONI TAARIFA YA VYETI FEKI VYA POLISI



Katika siku za hivi karibuni, kumeibuka tabia ya baadhi ya watu kutoa taarifa za uzushi na uongo kutumia majina ya taasisi, mashirika ya umma na ofisi za Serikali na kueneza taarifa hizo katika mitandao ya kijamii kwa lengo la kupotosha wananchi.

Miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na taarifa kuhusu Jeshi la Polisi iliyosambazwa jana katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari ‘chujio Jesho la polisi, vyeti feki vyawaonndoa askari kazini’ Taarifa hiyo ni uzushi na haijatolewa na Jeshi la Polisi.

Kufutia hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini linapenda kukanusha taarifa hiyo ya uzushi ambayo haina ukweli wowote na inalengo la kuchafua taswira ya Jeshi la Polisi kwa jamii.

Jeshi la Polisi nchini limeanza upelelezi wa kuwatafuta watu wote waliohusika kueneza taarifa hiyo na kujifanya wao ni Jeshi la Polisi.

Aidha, Tunatoa onyo kali kwa watu wote kuacha kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kufanya uposhaji na badala yake watumie mitandao hiyo kwa ajili ya ustawi wa jamii.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba – SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.

Chanzo- Udakuspecially.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post