Hii taarifa imechukua nafasi kubwa sana kwenye mitandao ya kijamii hasa kwenye Whatsapp, Instagram na Facebook pia… inaonekana gari ya magazeti imepata ajali na kunatajwa kuwa kuna watu wamefariki pia kwenye ajali hiyo.
Nimempata Mhariri wa gazeti la Mwananchi, Frank Sanga ambaye amesema yuko mkoani Tanga kikazi lakini taarifa alizozipata ni kwamba gari lililopata ajali ni gari ambalo lilikodiwa na Kampuni hiyo ya Magazeti kupeleka Magazeti Mbeya… mazingira ya ajali inaonesha gari hilo liligonga lori kwa nyuma, na madereva wote wawili waliokuwa ndani ya gari wamefariki.
Ajali hiyo imetokea maeneo ya mlima Kitonga mkoa wa Iringa.
#RIP kwa marehemu wa ajali hiyo.
Social Plugin