MAHAKAMA KUU YARIDHIA DHAMANA YA VIGOGO WA TRA WENYE KESI YA MAKONTENA 329 BANDARINI



Mahakama kuu ya Tanzania imeridhia dhamana kwa washitakiwa watatu wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA wanaokabiliwa na mashitaka ya kutoa makontena 329 bandarini bila kulipiwa kodi na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 12.7. 
 
 
Maamuzi hayo ya mahakama kuu ya Tanzania yamekuja kufuatia ombi la dhama lililowakilishwa mahakamani hapo na washtakiwa watatu wakiongozwa aliyekuwa kamishina wa forodha wa TRA Bw Tiagi Masamaki, ambapo kwa mujibu wa jaji wa mahakama hiyo Bi Wilfrida Koroso amesema dhamana kwa washitakiwa hao watatu iko wazi kama watatimiza masharti sita yakiwemo ya kulipa hundi ya shilingi bilioni 2.6 kila mmoja huku pia wakitakiwa kuwasilisha hati zao za kusafiri huku pia wakitakiwa kuwa na wadhamini watakao kuwa na uwezo wa kusain hundi ya shilingi milioni 20 kila mmoja.

Katika hatua nyingine mbunge wa jimbo la Ubungo Mh Saed Kubenea amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu Dar es Salaam akikabiliwa na shitaka la kutumia lugha ya matusi kinyume na sheria.

Akisoma shitaka mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo Thomas Simba, mwendesha mashitaka wa serikali Timon Vitalis ameiambia mahakama kuwa mnamo Dec 14 mwaka huu katika eneo la EPZ mtuhumiwa huyo alitumia lugha ya matusi" we kibaka, we mjinga, mpumbavu, cheo chenyewe umepewa" maneno yaliyokuwa yakimlenga mkuu wa wilaya ya Kinondoni, ambapo kwa mujibu wa mwendesha mashitaka huyo amesema maneno hayo yangeweza kuhatarisha amani ikiwa ni kwa mujibu wa kifungu namba 89 (i) A cha kanuni ya adhabu sura namba 16 ya mwaka 2002 ambapo hata hivyo mshitaka huyo alikana shitaka hilo.

Mtuhumiwa huyo alikuwa akitetewa na jopo la mawakili watano wakiongozwa na wakili Peter Kibatala ambapo hata hivyo baada ya kukidhi vigezo vya dhamana aliachiwa nje kwa dhamana.
 
Via>>Itv

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post