Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Mapenzi Noma!! MUME AUA MKE WAKE KWA MAPANGA KISHA NAYE KUJINYONGA





Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.


Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanaume mmoja Mkazi wa kijiji cha Malolo Ndugu Chipunguli Mkisi (30) amemuua mke wake kwa kumkata panga kichwani kisha yeye mwenyewe kujiua kwa kujinyonga.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ndugu Ahmed Msangi amesema tukio hilo la aina yake limetokea Desemba 15 mwaka huu majira ya saa 7 mchana huko katika kijiji cha Malolo, Kata ya Msia, wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Mbeya.


Msangi amemtaja mwanamke huyo kuwa ni Neva Mwaweza (24) Mkazi wa Malolo ambaye ameuwawa na mumewe kwa kukatwa panga kichwani .


Kamanda Msangi amesema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi baada ya mwanaume kumtuhumu mke wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.

Inadaiwa kuwa baada ya tukio, mtuhumiwa alijinyonga kwa kutumia kamba kwenye mti umbali wa mita 100 kutoka nyumbani kwake.

Aidha mwili wa marehemu [mwanaume] ulikutwa ukiwa na majeraha kwenye vidole na kando kukiwa na panga na alikutwa na ujumbe uliokuwa na maneno “kuwa ameamua kumuua mke wake na yeye kujinyonga kutokana na mke wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine aitwae Kilasi Nzowa”

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya Vwawa. ambapo kwa mujibu Kamanda Msangi uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Na Mwandishi wetu wa Jamiimojablog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com