WAZIRI wa Habari,Utamaduni,Wasanii na Michezo,Nape Nnauye amewatoa hofu wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini hususani Magazeti pamoja na wanahabari kwa kusema hatafungia magazeti badala yake atahakikisha anakuwa mlezi wa vyombo vya habari pamoja waandishi wa habari ili viweze kufanya kazi kwa weledi.
Akizungumza na wafanyakazi wa wizara ya Habari na utamaduni,wasanii na Michezo wakati alipokuwa akipokelewa na wafanyakazi wa wizara hiyo kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kwenye nafasi hiyo na Rais Magufuli, Nape amesema baada ya Rais Magufuli kumchagua kuwa Waziri wa wizara hiyo waliibuka watu wakisema magazeti yatafungiwa.
“Nawaomba watu wa sekta ya habari kuondoa dhana ya kwamba mimi nitakuwa mtu wa kuyafungia magazeti.Kitu kama hicho hakipo kwani nimekuja kwenye wizara hii ili wanahabri wafanye kazi kwa weredi .Ninawahahidi nitakuwa mlezi wa vyombo vya habari”amesema Nnauye.
Amesema anafahamu kwa sasa sheria ya magazeti ya mwaka 1976 imekuwa ikilalamikiwa sana,hivyo ameahidi kulishughulikia suala hill.
.
Hata hivyo Nape ambaye ni mbunge wa Jimbo la Mtama,amewaomba wanahabari pamoja na wamiliki kuhakikisha wanafanya kazi kwa weredi ili kuhakikisha wanaiweka jamii kwenye nafasi nzuri ya Amani kwa madai kuwa wanahabri wananafasi kubwa katika jamii ya kuilinda amani.
Kwa upande wake Naibu waziri wa wizara hiyo Anastazia Wambura amewataka watendaji wote wa wizara hiyo kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa ili waende sawa na jinsi Rais Magufuli anavyoenda na kasi ya kuwatumikia watanzania.
Lukuvi Akaribishwa Wizara ya Ardhi
Waziri wa Ardhi nyumba na maendelea ya Makazi,William Lukuvi ambaye amerejeshwa tena kwenye wizara hiyo baada ya uteuzi wa Rais Magufuli,amewataka viongozi wa wizara hiyo ndani ya siku saba wampelekee mipango mipya ya kiutendaji lasivyo mtendaji ambaye atashindwa kumpelekea taarifa ya mipango hiyo atafukuzwa kazi.
Waziri Lukuvi ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akikaribishwa tena na wafanyakazi wa wizara hiyo mara baada ya kurejeshwa tena na Rais Magufuli ambapo amesema kwa sasa anataka watumishi wote wafanye kazi kwa kasi ya Rais Magufuli huku akiwataka mpaka jumatatu wapeleke taarifa ya mipango kwa kila mtendaji wa wizara hiyo.
Amesema nia ya kuhitaji taarifa ya mipango hiyo ni kutaka kufahamu maeneo yapi muhimu kwa sasa kwa wananchi ili iwe rahisi kuwatumikia,
Sanjari na hilo Waziri Lukuvi ametoa kalipia kwa watu wote wanaomiliki mashamba ambayo wameshindwa kuyatekeleza kwa wakati na kusema kuwa wizara yake itahakikisha mashamba hayo wananyang’anywa na kurudishwa serikalini kwa ajili ya kupewa watu wengine wenye nia ya kuyatumia mashamba hayo.
Jaffo Naye Aibukia Bahi
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Utumishi na Utawala Bora, Selemani Jaffo amewatangazia kiama wakurugenzi wote nchini watakaoshindwa kuwasimamia wakuu wa idara katika Halmashauri zao.
Naibu huyo alitoa kauli hiyo jana alipofanya ziara yake ya kikazi ya kwanza ya kushtukiza katika wilaya ya Bahi iliyopo mkoani Dodoma.
Mbali na hilo ametoa muda wa siku 27 kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha zinatumia mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya kukusanya mapato katika halmashauri husika.
Jaffo amesema kwamba mfumo wa kizamani wa ukusanyaji mapato unachangia kwa kiasi kikubwa cha watumishi wengi pamoja na wakurugenzi kufanya ufisadi na kupiga fedha ya Umma.
Katika hatua nyingine amewaagiza watumishi wote katika halmashauri ya Bahi pamoja na halmashauri nyingine nchini kuhakikisha hawakai maofisini na badala yake watembelee miradi na kujua matatizo ya wananchi.
Amesema hakuna haja ya watumishi kukaa maofisini kwa ajili ya kusubiri taarifa ambazo wakati mwingine ni za upotoshaji na kusababisha wananchi kuichukia serikali yao.
Via>>>Mpekuzi blog
Social Plugin