Mgomo Dar!! WAFANYAKAZI WA KIWANDA CHA NGUO WAGOMA, WAPIGWA MABOMU,KIWANDA CHAFUNGWA
Thursday, December 03, 2015
Jeshi la Polisi Dar es Salaam leo limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki ambao walifanya mgomo na kuufungia uongozi wa kiwanda hicho ndani kwa madai ya kutolipwa ongezeko la mishahara yao kwa muda mrefu.
Uongozi wa wilaya ya Kinondoni umesitisha shughuli za uzalishaji katika kiwanda cha Urafiki baada ya viongozi wa kiwanda hicho kushindwa kuwalipa madai yao kama walivyokubaliana awali kuwa hadi Desemba mosi wangekuwa wameshalipwa.
Kutokana na Sekeseke hilo,Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ,Paul Makonda ameamuru kiwanda hicho kifungwe kwa muda ili kusaka suluhu .
Wafanyakazi hao ambao awali waligoma ili kushinikiza uongozi wa kiwanda hicho kuwalipa stahiki zao wamegoma tena hali iliyosababisha uongozi wa wilaya kuchukuwa hatua hiyo hadi wiki ijayo serikali itakapokuwa imelipatia ufumbuzi suala hilo. Mwandishi wetu amefika katika kiwanda hicho na kushuhudia wafanyakazi hao wakiwa wamefunga geti na kuweka kambi eneo hilo kwa madai kuwa uongozi wa kiwanda uwaeleze hatima ya malipo yao.
Kabla ya mkutano huo kumalizika katibu wa chama cha wafanykazi tawi la urafiki Bw Florian Makero ameeleza hatua mbalimbali walizochukuwa na wapi wamekwama kama anavyoeleza.
Hata hivyo katika hali ya kushangaza viongozi wote wa kiwanda hicho hawakuwepo maofisini na milango ilikuwa imefungwa hata baada ya viongozi wa serikali kufika.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin