Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MHESHIMIWA SUMAYE ATANGAZA RASMI KUHAMIA CHADEMA



Waziri mkuu wa awamu ya tatu Mh.Fredirick Sumaye amtangaza rasmi kujiunga na chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema na amekabidhiwa kadi na Mwenyekiti wa chama hicho Mh.Freeman Mbowe. 
 
Sumaye ambaye wakati wa uchaguzi alitangaza kujiondoa CCM na kudai kuwa anaunga mkono mageuzi yanayofanywa na vyama vinavyounda katiba ya wananchi (UKAWA) bila kuweka wazi kuwa yuko kwenye chama kipi kati ya hivyo amesema asa ameamua kujiunga na CHADEMA.

Akizungumza katika mkutano wa kufunga kampeni za ubunge wa jimbo la Arusha kwa chama cha CHADEMA uliofanyika kata ya baraa Sumaye amesema anataka kuungana na wanamageuzi wenzake katika kuendeleza harakati za mabadiliko hapa nchini ambazo bado zinaendelea.

Akizungumza baada ya kumkabidhi kadi Mwenyekiti wa chama hicho Mh.Freeman Mbowe amesema chadema na vyama washirika wa UKAWA bado viko imara na vimeendelea kuimarika na kwamba licha ya kudhulumiwa ushindi azma yaoya kuleta ukombozi nchini iko pale pale.

Awali aliyekuwa mgombea uras wa CHADEMA akiwakilisha vyama vya umoja wa katiba ya wananchi ukawa Mh.Edward Lowassa ameendelea kuwataka watanzania wanaounga mkono mabadiliko kuwa watulivu na kwamba kwa vile wana dhamira ya dhati ya kuyaona mabadiliko hakuna kukata tamaa kwani bado kuna fursa ya kufikiwa kwa malengo yao .
 Via>>ITV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com