Watu 12 wamefariki dunia papo hapo baada ya lori la mbao lililokuwa likitokea Njombe kwenda jijini Dar es Salaam kupasuka tairi na kugongana na basi la abiria la New Force lililokuwa linatokea jijini Dar es Salaam kuelekea Tunduma leo katika eneo la Kitonga wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, kamishina msaidizi wa polisi Ramadhani Mungi amesema waliofariki ni wanaume nane na wanawake wanne majeruhi ni 28 ambao wengine wamepelekwa Iringa mjini na wengine wako katika hospitali ya wilaya Kilolo-Iringa.
Aidha Kamanda Mungi amewataka madereva kuwa makini hasa katika kipindi hiki cha sikukuu na kuepuka mwendo kasi pamoja na kutoa taarifa pale vitendo kama hivyo vinapotokea
Social Plugin