Picha 37!! WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI TAWI LA KIZUMBI SHINYANGA WALIVYOADHIMISHA MIAKA 54 YA UHURU
Wednesday, December 09, 2015
Hapa ni katika Senta ya kijiji cha Nhelegani katika kata ya Kizumbi wilaya ya Shinyanga mkoa wa Shinyanga ambapo leo Desemba 09,2015 katika kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania bara wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga (Moshi Co Operative University(MOCU) wamefanya usafi wa mazingira katika kata ya Kizumbi kilichopo jirani na eneo la Chuo hicho kwa lengo la kuadhimisha miaka 54 ya uhuru na kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kufanya usafi sambamba na kutoa elimu kwa vitendo kwa wananchi kuwa suala la usafi ni kila mtu katika jamii.Wanafunzi hao kupitia Klabu yao ya Mazingira inayojulikana kwa jina la Enviro Care Club yenye wanachama zaidi ya 40 wamefanya usafi katika kijiji hicho kwa kuokota taka na kuchoma moto taka .Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio..ametuletea picha 37 kutoka eneo hilo..Angalia hapa chini
Bango la Chuo cha MOCU lililopo jirani na kijiji cha Nhelegani katika kata ya Kizumbi
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakiwa katika senta ya kijiji cha Nhelegani wakikusanya takataka zilizokuwa zimezagaa katika eneo hilo leo asubuhi.Wanachama Enviro Care Club iliyoanzishwa mwaka 2013 katika chuo hicho huwa wanafanya usafi katika chuo chao kila siku ya Jumamosi na kutokana na mazingira ya chuo chao kuwa kisafi ndipo leo katika kuadhimisha miaka 54 ya uhuru wameamua kufanya usafi katika kijiji kilichopo jirani na chuo chao ili kuwaonesha mfano wananchi wa eneo hilo kuwa marafiki wa mazingira.Mbali na kufanya usafi pia wanachama wa klabu hiyo wanajihusisha na upandaji na utunzaji wa miti
Pamoja na kwamba vijana hao hawana vitendea kazi lakini wamejitahidi kukusanya taka katika senta ya Nhelegani iliyoko katika barabara ya Tinde-Shinyanga
Mwalimu mshauri wa klabu ya mazingira MOCU ambaye ni ndiyo aliyetoa wazo la kuanzishwa kwa klabu hiyo Anthony Gikuri akikusanya taka katika senta ya Nhelegani iliyopo karibu na barabara ya Shinyanga-Tinde..Gikuri amesema changamoto kubwa inayowakabili katika kutekeleza suala la usafi katika chuo chao ni ukosefu wa vitendea kazi ikiwemo mipira ya mikononi hivyo kuwaomba wadau wa usafi kuwasaidia vifaa kwa ajili ya usafi katika chuo hicho na maeneo jirani na chuo
Kushoto ni rais wa Chuo Kikuu cha Ushirika kituo cha Kizumbi Daniel Thomson Mtani akiwa na wanafunzi wa chuo hicho wakisanya taka kwa kutumia dhana duni ikiwemo fimbo na mifuko ya rambo laini ambapo amesema waliamua kufanya usafi katika kata ya Kizumbi ili kumuunga mkono rais Magufuli sambamba na kuonesha mfano kwa wananchi hao waliopo jirani na chuo hicho.
Kushoto ni Mwenyekiti msaidizi wa klabu ya mazingira ya chuo Kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Amon Theobard akifuatiwa na rais wa Mocu Daniel Thomson Mtani na mwenyekiti wa klabu hiyo ya mazingira Chauya Mohammed Mkwazu wakifanya usafi katika kata ya Kizumbi
Mwanachama wa klabu ya Mazingira chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga akichoma moto taka katika senta ya Nhelegani kata ya Kizumbi mkoani Shinyanga
Hapa ni karibu na barabara ya Tinde-Shinyanga wanafunzi wa Chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi
Marafiki wa mazingira kutoka chuo kikuu cha Mocu wakifanya usafi katika senta yaNhelegani jirani na chuo hicho
Wanachama wa Klabu ya Mazingira chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakiendelea kufanya usafi
Tunamalizia kufanya usafi
Baada ya kumaliza kufanya usafi wanachama wa Klabu ya Mazingira chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakaamua kupiga picha ya kumbukumbu
Wanachama wa Klabu ya Mazingira chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kufanya usafi katika kata ya Kizumbi
Tunapiga picha ya kumbukumbu
Baadhi ya wanafunzi wa MOCU wakielekea chuoni baada ya kumaliza kufanya usafi katika kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi mkoani Shinyanga
Wanachama wa Klabu ya Mazingira chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wakielekea chuoni baada ya kumaliza kufanya usafi katika kata ya Kizumbi
Picha ya kumbumbuku ---Chwaaaaa!!!
Baada ya Wanachama wa Klabu ya Mazingira katika chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi kumaliza kufanya usafi katika kijiji cha Nhelegani kilichopo jirani na chuo hicho,mwandishi wa habari wa Mtandao huu,Kadama Malunde aliamua kutembelea chuo hicho ili kujionea hali halisi ya mazingira ya chuo hicho...Angalia picha hapa chini
Marafiki wa Mazingira kuta MOCU wakiwa katika picha ya pamoja
Rais wa chuo kikuu cha Ushirika kituo cha Kizumbi Daniel Thomson Mtani (kushoto) akirejea chuoni na wanafunzi wenzake baada ya kumaliza kufanya usafi katika kijiji cha Nhelegani kilichopo jirani na chuo
Kushoto ni waziri mkuu wa chuo kikuu cha Ushirika tawi la Kizumbi Jackson Jonael Mphuru akirejea chuoni na wenzake baada ya kumaliza kufanya usafi katika kijiji cha Nhelegani
Hapa ni karibu na Maktaba ya chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga,wanachama wa Enviro Care Club akiwemo rais wachuo cha Ushirika kituo cha Kizumbi Daniel Thomson Mtani(kulia) na waziri mkuu wa chuo hicho Jackson Jonael Mphuru (kushoto) wakiwa chuoni baada ya kumaliza kufanya usafi
Hii ni sehemu ya kusomea katika kikuu cha Ushirika Moshi Kituo cha Kizumbi Shinyanga
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi Kituo cha Kizumbi Shinyanga wakiwa wamepumzika katika kijumba cha kusomea nje ya madarasa yao
Moja ya majengo katika chuo cha MOCU
Muonekano wa mazingira ya chuo cha MOCU
Ndani ya moja ya madarasa katika chuo cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi Shinyanga wenyewe wanaita Nkurumah Hall
Mazingira ya chuo hicho kilichozungukwa na miti na maua ya kila aina
Hili ni jengo la Zahanati ya chuo hicho
Marafiki wa mazingira chuo cha MOCU wakiwa chuoni
Kulia ni mwenyekiti waya mazingira chuo kikuu cha Ushirika Moshi tawi la Kizumbi mkoani Shinyanga Chauya Mohammed Mkwazu akiwa katika shamba la kukuzia miti ambapo asema klabu yao inahusika na utunzaji wa mazingira pia upandaji na utunzaji wa miti hivyo zoezi la usafi kwao ni endelevu na sasa wameanza kuhamasisha wananchi wanaozunguka chuo chao wawe mstari wa mbele kutunza mazingira yao.
Jengo la Utawala
Waziri mkuu wa chuo kikuu cha Ushirika tawi la Kizumbi Jackson Jonael Mphuru katika pozi katika chuo hicho
Moja ya barabara katika chuo cha MOCU-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin