Desemba 02,2015- Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameendelea na ziara za kushtukiza kwenye maeneo ambayo ni kero katika wilaya hiyo.Ilikuwa majira ya saa tano asubuhi,mkuu huyo wa wilaya akaabukia katika soko kuu la manispaa ya Shinyanga lililojengwa kabla ya uhuru wa Tanganyika..Ikawa faraja kwa Wafanyabiashara wa soko hilo waliodai kwa kipindi kirefu wamekuwa wakiilalamikia halmashauri ya manispaa kutokana na kushindwa kulifanyia ukarabati soko hilo.Akiwa katika soko hilo Josephine Matiro amesikiliza kero nyingi kutoka kwa wafanyabiashara hao ikiwemo ukosefu wa mitaro,kalo la maji,uchafu sokoni.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio..Anatusimulia kwa picha 40 kilichojiri mwanzo hado mwisho..Tazama hapa chini
Ndani ya soko kuu la manispaa ya Shinyanga viazi vikiwa chini pembeni maji machafu
Hili ni soko la manispaa ya Shinyanga/mkoa wa Shinyanga lililojengwa zaidi ya miaka 50 iliyopita
Ndani ya soko kuu mjini Shinyanga
Afisa Masoko wa manispaa ya Shinyanga Mabina Sang'udi (wa pili kutoka kushoto) akitoa maelezo namna wafanyabishara wanavyokiuka taratibu za sokoni na kufanya soko lionekane halifai
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa ndani ya soko kuu mjini Shinyanga,pichani juu kulia ni viatu ambavyo kimsingi havipaswi kuuzwa katika soko hilo ambalo ni maalum kwa bidhaa zinazotoka shambani tu
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia ghuba la taka katika soko hilo
Uchafu katika ghuba la soko kuu mjini Shinyanga,wazoa uchafu wakitumia nyenzo duni
Mkuu wa wilaya alifika pia katika choo cha soko hilo kinacholalamikiwa kutokuwa kisafi ingawa mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna amedai ni kisafi na kuupongeza uongozi wa soko hilo.Hata hivyo wafanyabiashara hao walisema kumekuwa na bei tofauti tofauti ukitaka kujisaidia wakati mwingine unatozwa shilingi 200,300 au 100.
Moja ya matundu ya vyoo katika soko hilo.Kwa mujibu wa afisa biashara wa manispaa ya Shinyanga Sande Deogratius bei ya kujisaidia katika vyoo hivyo ni shilingi 300/= kwa haja kubwa,haja ndogo shilingi 200/=
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akitoka kukagua choo ,kulia kwake ni afisa mtendaji wa kata ya Shinyanga mjini Mathias Masalu
Mfanyabishara akiuza dagaa na makopo,ndoo tupu ndani ya soko
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna wakiangalia mifuko yenye chupa na makopo ndani ya soko la bidhaa za mashambani,ambapo waliagiza mifuko,maboksi,chupa na vingine vyote visivyotakiwa kuondolewa sokoni
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna(mwenye nguo nyeusi) akitoa maelekezo kwa afisa masoko wa manispaa ya Shinyanga kuhakikisha kuwa kero za soko hilo zinatatuliwa haraka iwezekanavyo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika eneo la kalo la maji machafu(kulia) lililojaa na kufunikwa maboksi hali ambayo ni hatari kwa afya za wafanya biashara wa soko hilo.Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyang Lewis Kalinjuna aliahidi kukarabati kalo hilo kuanzia wiki ijayo
Afisa Masoko manispaa ya Shinyanga Mabina Sang'undi akisisitiza jambo kwa mkuu wa wilaya na msafara wake
Mifuko ya makopo na chupa sokoni
Badala ya kuuza bidhaa za shambani,sasa wanauza na chupa kabisaa
Paa likiwa limetoboka katika chumba cha mama lishe sokoni,ambacho pia uongozi wa manispaa uliahidi kufanya ukarabati
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoka kwenye chumba cha mama ntilie sokoni
Mama Ntilie akipika katika eneo la wazi kutokana na kukosa nafasi sokoni hapo
Mama Lishe akieleza kero kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,ambapo alisema hawana eneo la kupikia matokeo yake wateja wanakimbia wakati wanalipa ushuru shilingi 300 kila siku
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga wakishangaa jinsi soko lilivyo chafu
Mkuu pita na huku uone......
Bidhaa zikiwa sokoni
Ndani ya soko kuu mjini Shinyanga
Hapa ni nje ya soko biashara inaendelea,wenyewe wanadai hakuna sehemu ya kuuzia ndani ya soko...uongozi wa manispaa ya Shinyanga umeanza zoezi la kukamata wauza matunda wanaofanya biashara nje ya soko na barabarani na kutaka wafanyie biashara zao sokoni
Baada ya kutembelea soko hilo,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akafanya kikao na wafanyabiashara wa soko hilo,alimuagiza afisa masoko wa manispaa hiyo Mabina Sang’udi kuhakikisha uchafu wote ambao uko ndani ya maboksi pamoja na chupa tupu kuondolewa ili soko liwe katika mpangilio mzuri tofauti na hali ilivyo sasa hakuna mpangilio mzuri. |
Mfanyabiashara Isack
Ngolita akizungumzia kero katika soko hilo ambapo alisema soko
hilo halina mpangilio mzuri kutokana na kutotenganishwa
sehemu za kuuzia bidhaa zao
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,mkurugenzi wa mamispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna wakisikiliza kero za wafanyabiashara sokoni
Afisa afya wa manispaa ya Shinyanga Heri Nakuzelwa akizungumza
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna akizungumza katika kikao hicho
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,mkurugenzi wa mamispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna wakisikiliza kero za wafanyabiashara sokoni
Afisa afya wa manispaa ya Shinyanga Heri Nakuzelwa akizungumza
Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna akizungumza katika kikao hicho
Mkurugenzi
wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna alisema
uboreshaji wa soko hilo utaanza kutekelezwa
haraka ikiwamo kujenga upya shimo la maji machafu
ambalo litawekewa chujio ,kuweka mpangilio mzuri na
kuanza ujenzi wa mitaro ili maji
yaweze kutiririka na kuondoa kero kwa
wafanyabiashara.
Mwenyekiti
wa wafanyabiashara wa soko hilo Alex Stephen akizungumza baada ya kuundwa kwa kamati maalum kwa ajili ya kutatua kero za wafanyabishara sokoni
Wafanyabishara wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Eneo la mkutano
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wafanyabiashara wa soko kuu mjini Shinyanga
Wafanyabishara wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Eneo la mkutano
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wafanyabiashara wa soko kuu mjini Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiondoka sokoni-Picha zote na Kadama Malunde -Malunde1 blog |
ANGALIA Picha 37!! MKUU WA WILAYA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA VYOO MANISPAA YA SHINYANGA..AKUTANA NA VYOO VYA AJABU...KIMO CHA KULENGA KWENYE BOMBA