Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha 40!! MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA AFANYA ZIARA SOKO KUU SHINYANGA,MAZINGIRA YA SOKO YANATISHA



Desemba 02,2015- Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ameendelea na ziara za kushtukiza kwenye maeneo ambayo ni kero katika wilaya hiyo.Ilikuwa majira ya saa tano asubuhi,mkuu huyo wa wilaya akaabukia katika soko kuu la manispaa ya Shinyanga lililojengwa kabla ya uhuru wa Tanganyika..Ikawa faraja kwa Wafanyabiashara wa soko hilo waliodai kwa kipindi kirefu wamekuwa wakiilalamikia halmashauri ya manispaa kutokana na kushindwa kulifanyia ukarabati soko hilo.Akiwa katika soko hilo Josephine Matiro amesikiliza kero nyingi kutoka kwa wafanyabiashara hao ikiwemo ukosefu wa mitaro,kalo la maji,uchafu sokoni.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio..Anatusimulia kwa picha 40 kilichojiri mwanzo hado mwisho..Tazama hapa chini

Mkuu wa wilaya ya Shinyang Josephine Matiro akiwa na mwenyekiti wa soko kuu mjini Shinyanga Alex Stephen ambaye alisema kwa muda mrefu kumekuwa na kero ikiwemo ukosefu wa mitalo ya kupitishia maji machafu,kalo la maji machafu kujaa,ghuba la taka kujaa mara kwa mara.Alisema licha ya kwamba wataalamu wa halmashauri walishafanya tathmini ya namna ya kujenga mitaro lakini hakuna utekelezaji uliofanyika huku wao wakiendelea kupata kero wakati wanalipa ushuru na michango mingine inayohitajika.


Ndani ya soko kuu la manispaa ya Shinyanga viazi vikiwa chini pembeni maji machafu



Hili ni soko la manispaa ya Shinyanga/mkoa wa Shinyanga lililojengwa zaidi ya miaka 50 iliyopita


Ndani ya soko kuu mjini Shinyanga

Afisa Masoko wa manispaa ya Shinyanga Mabina Sang'udi (wa pili kutoka kushoto) akitoa maelezo namna wafanyabishara wanavyokiuka taratibu za sokoni na kufanya soko lionekane halifai

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa ndani ya soko kuu mjini Shinyanga,pichani juu kulia ni viatu ambavyo kimsingi havipaswi kuuzwa katika soko hilo ambalo ni maalum kwa bidhaa zinazotoka shambani tu

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiangalia ghuba la taka katika soko hilo

Uchafu katika ghuba la soko kuu mjini Shinyanga,wazoa uchafu wakitumia nyenzo duni



Mkuu wa wilaya alifika pia katika choo cha soko hilo kinacholalamikiwa kutokuwa kisafi ingawa mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna amedai ni kisafi na kuupongeza uongozi wa soko hilo.Hata hivyo wafanyabiashara hao walisema kumekuwa na bei tofauti tofauti ukitaka kujisaidia wakati mwingine unatozwa shilingi 200,300 au 100.


Moja ya matundu ya vyoo katika soko hilo.Kwa mujibu wa afisa biashara wa manispaa ya Shinyanga Sande Deogratius bei ya kujisaidia katika vyoo hivyo ni shilingi 300/= kwa haja kubwa,haja ndogo shilingi 200/=

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga akitoka kukagua choo ,kulia kwake ni afisa mtendaji wa kata ya Shinyanga mjini Mathias Masalu

Mfanyabishara akiuza dagaa na makopo,ndoo tupu ndani ya soko

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna wakiangalia mifuko yenye chupa na makopo ndani ya soko la bidhaa za mashambani,ambapo waliagiza mifuko,maboksi,chupa na vingine vyote visivyotakiwa kuondolewa sokoni



Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna(mwenye nguo nyeusi) akitoa maelekezo kwa afisa masoko wa manispaa ya Shinyanga kuhakikisha kuwa kero za soko hilo zinatatuliwa haraka iwezekanavyo



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa katika eneo la kalo la maji machafu(kulia) lililojaa na kufunikwa maboksi hali ambayo ni hatari kwa afya za wafanya biashara wa soko hilo.Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyang Lewis Kalinjuna aliahidi kukarabati kalo hilo kuanzia wiki ijayo



Afisa Masoko manispaa ya Shinyanga Mabina Sang'undi akisisitiza jambo kwa mkuu wa wilaya na msafara wake




Mifuko ya makopo na chupa sokoni



Badala ya kuuza bidhaa za shambani,sasa wanauza na chupa kabisaa



Paa likiwa limetoboka katika chumba cha mama lishe sokoni,ambacho pia uongozi wa manispaa uliahidi kufanya ukarabati




Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akitoka kwenye chumba cha mama ntilie sokoni



Mama Ntilie akipika katika eneo la wazi kutokana na kukosa nafasi sokoni hapo




Mama Lishe akieleza kero kwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga,ambapo alisema hawana eneo la kupikia matokeo yake wateja wanakimbia wakati wanalipa ushuru shilingi 300 kila siku



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga na mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga wakishangaa jinsi soko lilivyo chafu



Mkuu pita na huku uone......



Bidhaa zikiwa sokoni



Ndani ya soko kuu mjini Shinyanga



Hapa ni nje ya soko biashara inaendelea,wenyewe wanadai hakuna sehemu ya kuuzia ndani ya soko...uongozi wa manispaa ya Shinyanga umeanza zoezi la kukamata wauza matunda wanaofanya biashara nje ya soko na barabarani na kutaka wafanyie biashara zao sokoni

Baada ya kutembelea soko hilo,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akafanya kikao na wafanyabiashara wa soko hilo,alimuagiza  afisa  masoko  wa manispaa hiyo  Mabina  Sang’udi  kuhakikisha  uchafu wote ambao uko ndani ya maboksi  pamoja  na chupa tupu   kuondolewa  ili soko  liwe  katika  mpangilio  mzuri  tofauti  na hali  ilivyo  sasa  hakuna  mpangilio  mzuri.


Askari polisi wakiwa eneo la tukio

Mkutano unaendelea


Mfanyabiashara Isack  Ngolita akizungumzia kero katika soko hilo ambapo alisema soko  hilo halina mpangilio mzuri  kutokana na  kutotenganishwa  sehemu  za  kuuzia  bidhaa  zao
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,mkurugenzi wa mamispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna wakisikiliza kero za wafanyabiashara sokoni

Afisa afya wa manispaa ya Shinyanga Heri Nakuzelwa akizungumza

Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna akizungumza katika kikao hicho



Mkurugenzi  wa manispaa  ya Shinyanga  Lewis Kalinjuna   alisema  uboreshaji  wa  soko  hilo  utaanza  kutekelezwa  haraka  ikiwamo  kujenga  upya  shimo la maji machafu ambalo litawekewa  chujio  ,kuweka mpangilio  mzuri  na kuanza  ujenzi  wa  mitaro  ili  maji  yaweze  kutiririka  na kuondoa  kero  kwa  wafanyabiashara.



Mwenyekiti  wa wafanyabiashara wa soko  hilo  Alex    Stephen akizungumza baada ya kuundwa kwa kamati maalum kwa ajili ya kutatua kero za wafanyabishara sokoni
Wafanyabishara wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea

Eneo la mkutano

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wafanyabiashara wa soko kuu mjini Shinyanga

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiondoka sokoni-Picha zote na Kadama Malunde -Malunde1 blog

ANGALIA Picha 37!! MKUU WA WILAYA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA VYOO MANISPAA YA SHINYANGA..AKUTANA NA VYOO VYA AJABU...KIMO CHA KULENGA KWENYE BOMBA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com