Leo Jumanne Desemba 08,2015,Madiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika manispaa ya Shinyanga wamempitisha tena aliyekuwa mstahiki Meya wa manispaa hiyo katika kipindi kilichopita, Gulam Hafiz Mukadam (pichani) kugombea tena nafasi hiyo katika uchaguzi wa baraza la madiwani wa manispaa hiyo.Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Mukadam (pichani)ameibuka na ushindi wa kishindo baada ya kupata kura 12 na kuwashinda wapinzani wake wawili, David Nkulila diwani wa kata ya Ndembezi aliyekuwa naibu meya katika kipindi kilichopia ambaye alipata kura 3 na Hassan Mwendapole ambaye pia amepata kura 3.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo wa kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi, katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini, Charles Sangula amesema kwa matokeo hayo, mgombea nafasi ya umeya katika baraza la madiwani manispaa ya Shinyanga kwa tiketi ya CCM atakuwa ni Mukadam.
Gulam Hafiz Mukadam akizungumza na Malunde1 blog baada ya kutangazwa kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi wa meya manispaa ya Shinyanga ambapo alisema atafanya kazi kwa kuendana na kasi ya rais John Magufuli ili kuwaletea maendeleo wananchi.Mukadam amewaahidi wakazi wa manispaa ya Shinyanga kuwa ataendeleza kasi ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo kama alivyoahidi katika kipindi cha kampeni za udiwani,na kuhakikisha anakamilisha viporo vyote vya miradi aliyoianzisha.
Gulam Hafiz Mukadam ambaye ni diwani wa kata ya Shinyanga Mjini akiendesha baraza la madiwani wa manispaa ya Shinyanga katika kipindi kilichopita-Picha kutoka Maktaba ya Malunde1 blog
Atakayegombea nafasi ya naibu Meya katika manispaa hiyo kupitia CCM ni diwani mteule wa kata ya Kolandoto, Agnes Machiya aliyepata kura 10 na kuwashinda wapinzani wake wawili, Juma Nkwabi aliyepata kura 4, na Moris Mgini ambaye pia aliambulia kura 4.Wakati huo huo katibu wa madiwani wa CCM aliyechaguliwa ni diwani wa viti maalum Mariamu Nyangaka aliyepata kura 10 na kumshinda mpinzani wake Picca Chongela aliyepata kura 8.
Taarifa tulizozipata ni kwamba aliyeteuliwa kugombea nafasi ya umeya kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) ni bwana Ntobi Emmanuel ambaye ni diwani wa kata ya Ngokolo.

Social Plugin