Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha! HII HAPA TAARIFA YA JESHI LA POLISI SHINYANGA KUHUSU SIKUKUU YA MAULID,CHRISMAS NA MWAKA MPYA 2016



 
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Mika Nyange akizungumza na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga leo asubuhi katika ukumbi wa jeshi la polisi,ambapo mbali na kujitambulisha kwa waandishi wa habari ikiwa ni siku chache tu baada ya kuchukua nafasi ya Kamanda Justus Kamugisha aliyehamishiwa mkoani Mwanza,amezungumzia kuhusu suala la ulinzi hasa katika kipindi hiki cha sikukuu ya Maulid,Krismas na Mwaka Mpya 2016.Taarifa ya jeshi la polisi ipo hapo chini ya picha zote-Picha zote na Kadama Malunde na Abeid Suleiman-Malunde1 blog




Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Mika Nyange amewataka wamiliki wa kumbi za starehe kutozidisha idadi ya watu katika maeneo yao wakati wa kusherehekea sikukuu za Maulid,Krismasi na mwaka mpya ili kuepeuka vitendo vya uhalifu kwani kuna baadhi ya watu hutumia fursa ya sikukuu kufanya uhalifu.





Kamanda Mika Nyange ametoa wito kwa wananchi
kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za mtu au watu wanaojihusisha na vurugu na fujo katika kipindi hiki cha sikukuu.




Waandishi wa habari wakiwa katika ukumbi wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga



Kulia ni mkuu wa upelelezi mkoa wa Shinyanga Mussa Athuman Taibu,kushoto ni Kamishna msaidizi wa jeshi la polisi ACP Dismas Kisusi,katikati ni kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACPMika Nyange




Waandishi wa habari wakiwa ukumbini



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com