Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John P. Magufuli, amemteua Valentino Mlowola, kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Lilian Mashaka aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Kabla ya Uteuzi Mlowola alikuwa ni Kamishna wa Polisi na Mkurugenzi Intelijensia ya Makosa ya Jinai katika Jeshi la Polisi.
Pia,kabla ya kuteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi na Mkurugenzi Intelejensia ya Makosa ya Jinai katika Jeshi la Polisi alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza.
Social Plugin