Dotto Mzava enzi za uhai wake
Wa pili kutoka kulia(waliosimama) ni Dotto Mzava akiwa na Bloggers wenzake nchini Tanzania walipokutana jijini Dar es salaam hivi karibuni.
Blogger chipukizi nchini Tanzania Dotto Mzava, amefariki Dunia katika ajali ya pikipiki leo Disemba 14, 2015 kufuatia ajali iliyohusisha pikipiki na gari iliyotokea maeneo ya Victoria, Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Taarifa za kifo cha Dotto Mzava zimethibitishwa na mwenyekiti Chama cha Blogu Tanzania (Tanzania Bloggers Network, TBN), Joachim Mushi Mzava,ambacho Dotto Mzava alikuwa ni mwanachama wake.
Dotto alikuwa akifanyia kazi Jamii Media Limited (Wamiliki wa mtandao wa Jamii Forum) na Mwandishi Mkuu wa FikraPevu.com
Mipango ya mazishi na kusafirisha mwili wa marehemu kuelekea kwao Same kwa ajili ya maziko inaendelea kufanyika na kwa sasa mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala. Kuaga mwili kwa wakazi wa Dar kutafanyika Disemba 17, 2015 katika Kanisa la Waadventista Wasabato, Manzese (ulipo uwanja wa Tippi).
R.I.P Dotto Mzava
Social Plugin