Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

UTPC YAANZA KUGAWA VIFAA VYA OFISI KWA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI NCHINI TANZANIA




Zoezi la ugawaji wa vifaa kwa ajili ya klabu za waandishi wa habari nchini limeanza rasmi katika ofisi za Muungano wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania-UTPC jijini Mwanza , ambapo leo UTPC imegawa vifaa kwa klabu sita ambazo ni Mara Press Club, Kagera Press Club, Shinyanga Press Club, Mwanza Press Club, Tabora Press Club na Central Press Club.
Klabu zingine zitagawiwa vifaa mbalimbali vya ofisi kulingana na ratiba itakavyopangwa.Pichani mwenye nguo nyekundu ni Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Abubakar Karsan akizungumza na wawakilishi wa Klabu hizo ofisini kwake kabla ya kuanza kwa zoezi la ugawaji wa vifaa hivyo katika ofisi za UTPC jijini Mwanza leo.Vifaa vilivyogawanywa ni pamoja na meza moja ya ofisi pamoja na viti vitatu, ambapo zoezi hilo litaendelea kwa klabu zingine 27 kote nchini




Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Bw. Abubakar Karsan Abubakar Karsan akiangalia vifaa tayari kwa kuvigawa ambapo zoezi la kukabidhi samani za ofisi kwa wawakilishi wa klabu 6 za waandishi wa habari katika mikoa ya Mara, Kagera, Shinyanga, Dodoma, Mwanza na Tabora , zoezi lililofanyika katika ofisi za UTPC jijini Mwanza.



Afisa Programu Utawala na Manunuzi wa UTPC Bi Hilda Kileo akitoa maelezo kuhusiana na vifaa hivyo

Kushoto ni mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (SPC) ,Kadama Malunde akipokea kiti kutoka kwa mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Abubakar Karsan


Mkurugenzi mtendaji wa UTPC Abubakar Karsan akikabidhi kiti kwa katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Tabora  Paul Malimbo
Katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Mara Pendo Mwakyembe  akipokea kiti



Mkurugenzi Mtendaji WA UTPC akimkabidhi kiti Makamu Mwenyekiti wa Press Club ya Kagera Jane Novert



Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Bw. Abubakar Karsan akimkabidhi vifaa Makamu Mwenyekiti wa Central (Dodoma) Press Club Bi Rachael Chibwete



Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC Bw. Abubakar Karsan akimkabidhi kifaa Mweka Hazina wa Mwanza Press Club Bi  Paulina David

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com