Aliyekuwa kamishina msaidizi wa jeshi la polisi nchini Hussein Kashindye(pichani) amefariki dunia katika hospitali ya Maweni mkoani Kigoma.
Taarifa tulizozipata ni kwamba Kashindye alikuwa mkoani Kigoma kwa kazi maalum ya jeshi la polisi lakini wakati akiendelea kutekeleza majukumu yake hali ilibadilika na kukimbizwa katika hospitali ya Maweni na taarifa zinadai kuwa amefariki dunia jana usiku kwa ugonjwa wa shinikizo la damu.
ACP Hussein Kashindye alikuwa akifanya kazi makao makuu ya polisi Dar es salaam.
Kabla ya kuhamishiwa jijini Dar es salaam,Kashindye alikuwa mkuu wa upelelezi wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga.
Taarifa tulizozipata ni kwamba mazishi yanatarajia kufanyika kesho Alhamis nyumbani kwao Lunguya wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
R.I.P Kashindye
ACP Hussein Kashindye enzi za uhai wake akiwajibika-picha kutoka Maktaba yetu
ACP Hussein Kashindye akizungumza katika siku ya wadau wa habari mkoa wa Shinyanga mwaka 2014-picha kutoka maktaba ya Malunde1 blog
ACP Hussein Kashindye kulia mbele mwenye suti akiwa waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali wa habari siku ya wadau wa habari mkoa wa Shinyanga mwaka 2014-picha kutoka maktaba ya Malunde1 blog
Social Plugin