Abiria moja amefariki na wengine wanne wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Iramba, baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kugonga kingo za daraja katika mlima Sekenke wilayani Iramba.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida ACP Simoni Haule amesema ajali hiyo ambayo imehusisha basi la Mohamed Trans lenye usajili wa namba T.858 AWY Scania iliyokuwa ikitokea Mwanza na kuelekea jijini Dar-es-Salaam, baada ya kugonga kingo ya daraja katika mlima Sekenke wilayani Iramba.
Katika hatua nyingi kamanda Haule amesema chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya usukani wa basi hilo na hivyo kupelekea dereva wa basi hilo Bwana Jovin kushindwa kulimudu na kugonga kingo za barabara na kusababisha kifo na majeruhi.
Kamanda Haule amewataka madereva na wamiliki wa mabasi kuwa makini kuhakikisha mabasi yao wana yafanyia matengenezo mara kwa mara.
Chanzo-ITV
Social Plugin