Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BANGO HILI LAZUA BALAA KWENYE SHEREHE ZA MAPINDUZI YA ZANZIBAR LEO, ZITTO KABWE AKEMEA, CCM WALAANI VIBAYA



Hili ndiyo bango lililolaniwa na CCM




TAARIFA KWA UMMA



Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesikitishwa sana na ujumbe wenye maudhui ya ubaguzi ulioandikwa kwenye moja ya Bango lililobebwa na mmoja wa wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaomba radhi kwa ujumbe huo, kinapinga na kinakemea kabisa fikra, hisia na mitazamo yoyote yenye maudhui ya kibaguzi.


Ujumbe huo sio tu kuwa una maudhui ya kibaguzi bali pia unaenda kinyume kabisa na falsafa na Shabaha ya waasisi wa Mapinduzi hayo Matukufu ya mwaka 1964 na unapingana na misingi na itikadi ya CCM inayohimiza Umoja na Mshikamano wa Kitaifa.

Daniel Chongolo
Mkuu wa Mawasiliano na Umma CCM.
12/01/2016


Kabla ya CCM Kuomba Radhi,Mwanasiasa nguli nchini Tanzania Zitto Kabwe alipost picha ya bango Hilo hapo juu na ujumbe ufuatao katika ukurasa wake wa Facebook



" Siasa za. Hatari sana hizi. Siasa za kibaguzi. Siasa zinazopaswa kulaaniwa na kila mpinga ubaguzi nchini. Nitashangaa sana kama wakubwa CCM hamtaomba radhi kwa siasa hizi hizi mbaya kabisa. What will be the stop?"

FUATILIA ZAIDI HAPA..BOFYA HAPA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com