Mpiga picha Dennis Mallari raia wa Ufilipino alikuwa na jukumu moja tu siku ya mkesha wa mwaka mpya ndani ya Dubai… kazi yake ilikuwa kuhakikisha anapata picha kali za fataki zitakazopigwa angani usiku wa mkesha wa kuupokea mwaka 2016 katika ghorofa refu Dubai, Burj Khalifa.
Kwa bahati mbaya akiwa kwenye ghorofa ya 48 jengo la Hoteli ya Address Downtown, alishtukia kulipuka kwa moto mkubwa ghorofa ya 28 huku moto huo ukiendelea kuwaka kuelekea ghorofa za juu.
Moto huo ulifanya vyumba vingi vya hoteli kujaa moshi na ikashindikana kabisa jinsi ya mpigapicha huyo kutoka nje… Baada ya hali kuwa ngumu na kujikuta hana msaada wowote aliamua kupost ujumbe kwenye ukurasa wake wa Facebook kuomba msaada.
Baada ya kama saa mbili bila msaada wowote, mpiga picha huyo aliamua kutoka dirishani kwa kuning’inia kwenye kamba za mashine ya kusafishia madirisha mpaka alipopata msaada wa jamaa wa kikosi cha zimamoto ambao walimwokoa.
Stori ya jamaa mwenyewe hii hapa kutoka CNN.