Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Kali ya Kuanzia Mwaka!! JAMAA AIBA NYOKA NA KUMFICHA SEHEMU ZAKE ZA SIRI,VIDEO IKO HAPA



Hivi unaanzaje kuleta mzaha na nyoka mtu wangu ?! Eti nyoka unamuiba na bado unamficha kwenye nguo ya ndani uliyovaa ???


Mama mmiliki wa duka linalouza nyoka pamoja na wadudu wengine la A to Z Pets lililopo Portland, Oregon Marekani analalamika tu kitendo cha jamaa huyo aliyeingia kama anachekicheki hivi ahudumiwe alafu akatoka na nyoka aliyemuiba na kumficha kwenye nguo ya ndani aliyovaa karibu kabisa na sehemu zake za siri.

Mama huyo Christin Bjugan amelalamika kwamba nyoka wao mwenye thamani ya kama dola 200 hivi kaibiwa na jamaa huyo, kilichosaidia akamgundua mwizi wake ni camera za CCTV alizozitega ndani ya duka lake.

Unaweza kuona tukio lote lililonaswa na CCTV mpaka jamaa anapoiba nyoka kwa kumuingiza kwenye nguo ya ndani.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com