Matukio matatu ya watu kuuawa hutokea kila mwezi Wilaya Mlele Mkoani Katavi kwa kukatwa katwa na mapanga katika maeneo wanayoishi Wafugaji.
Hayo yalisemwa hivi karibuni na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali mstaafu Issa Njiku wakati akisoma taarifa ya Serikali ya Wilaya ya Mlele kwa Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Wiliam Ole Nasha kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mlele.
Alisema matukio ya mauaji yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara Wilayani hapo ni mauaji ya watu katika maeneo ya wanako ishi Wafugaji wa mifugo ya Ng’ombe.
Aliyataja maeneo ambayo mauaji hayo yamekuwa yakitokea ni katika Tarafa za Mpimbwe na Mamba katika Halmashauri ya Mpimbwe Ndurumo katika Halmashauri ya Nsimbo na Inyonga katika Halmashauri ya Mlele.
Kanali Njiku alimweleza Naibu Waziri kuwa kila mwezi hutokea matukio matatu ya watu kuuawa kwa kukatwa katwa na mapanga Wilayani humo.
Alisema katika kukabiliana na hari ya matukio hayo Serikali ya Wilaya imeweka mikakati ya kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama Wilayani humo inakuwa shwari.
Alisema na wameendelea kusisitiza suala la polisi jamii katika katika kila Kata na kuwataka Wananchi wanapowakamata wahalifu au majambazi kutotumia sheria mikononi badala yake wawafikishe wahalifu Polisi kwa hatua za kisheria.
Naibu Waziri Nasha aliwataka viongozi wa Wilaya hiyo waakikishe wanaweka utaratibu wa kuzia watu kuhamia kiholela na wahakikshe watu wanao hamia wanafata taratibu za kisheria.
Alisema lengo la Serikali sio kuwazuia watu kuhamia kwenye maeneo mengine cha msingi ni watu wanahamia kwenye maeneo wafuate utaratibu na sheria.
Aidha Nasha aliwataka viongozi wa Wilaya ya Mlele kutenga maeneo ya ardhi kwa shughuli mbalimbali ili kuepukana na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikitokea mara kwa mara.
Na Walter Mguluchuma-Malunde1 blog Katavi